Watu wawili wamekamatwa na
Polisi wakihusishwa na shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa
'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.
Shambulizi hilo liliyokea siku ya jumatatu saa nne usiku.
Watu wasiojulikana walirusha bomu
ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja
kati yao akiwa na majeraha makubwa.
Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20
wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na
mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa
Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment