EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 11, 2014

DEREVA: SITOI RUSHWA LABDA UNIUE!


CHANZO NI GPL SEKESEKE la aina yake kati ya dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up na trafiki ambao majina yao hayakujulikana mara moja liliibuka na kuzua maswali mengi kwa mashuhuda huku mambo ya rushwa yakitajwatajwa.
Trafiki akimdhibiti dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up.
Tukio hilo lilizozua maswali mengi liliibuka juzi Jumatano, Bamaga, Mwenge jijini Dar jirani na kituo cha mafuta cha Bamaga.

Katika tukio hilo, dereva huyo na trafiki walikuwa wakikunjana, ambapo dereva alikuwa akilalamika kuonewa (Haikujulikana kivipi) wakati askari huyo wa usalama barabarani akisisitiza kuwa jamaa huyo alivunja sheria.
Gari aina ya 'Land Rover' (break down) lililotumika kuvuta gari la aina ya Toyota Pick up la dereva huyo. 
ILIKUWAJE?
Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, kikiwa katika pitapita zake za kusaka matukio na kuhakikisha maadili hayavunjwi ndipo kilipokutana na kisanga hicho cha kushangaza.
Trafiki alisikika akimwambia dereva kuwa amevunja sheria za barabarani huku gari lake likiwa bovu hivyo aliamuru gari hilo kuvutwa hadi kituoni kwa ajili ya ukaguzi lakini dereva huyo alikataa.

...ilikuwa ni vigumu sana kwa dereva huyo kukubali gari lake kukamatwa.
DEREVA
Pamoja na kuelezwa kuwa gari lake lilikuwa na matatizo na mahali alipoegesha hapakuwa sahihi, dereva huyo alipayuka: “Nawajua nyie trafiki, kazi yenu ni kuonea watu sasa mimi sitoi kitu hapa, labda mniue.“Siendi popote, mkiondoa gari nalala mbele yake ili mnigonge nife, mimi nimesema silitoi.”

...dereva akizidi kubisha kwa uamuzi uliochukuliwa na afisa usalama wa barabarani 'trafiki' .
TRAFIKI
Trafiki huyo aliyeonekana kuwa makini na kazi yake, hakuwa na makuu, zaidi alitaka gari livutwe hadi kituoni huko sheria ingefuata mkondo wake baada ya ukaguzi.

Mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia Ijumaa kuwa, kilichohitajika ilikuwa ni busara ya masikilizano kuliko kuvutana kwa maneno na afisa wa polisi.
Afisa usalama wa barabarani akisisitiza kulichukua gari la dereva huyo kwa ukaguzi zaidi.
“Sasa kama gari lake anajua ni zima, anabishana nini na polisi? Ikiwa anajiamini kuwa aliegesha sehemu sahihi, hofu yake ni nini? Kama kweli anajua yupo sawa, anatakiwa kukubali kwenda polisi, gari likakaguliwe.
“Wakati mwingine unaweza kuwalaumu tu askari, kumbe ni tabia ya watu kukataa kutii sheria bila shuruti. Sasa anafikiri kwa maneno makali anayotoa kwa huyo askari atamwachia?
Raia wakishuhudia mkasa huo uliotokea katika kituo cha mabasi yaendayo Mwenge cha Bamaga.
“Anasema eti hatoi kitu, kwani kaombwa rushwa pale au anadhani kila trafiki anayemkamata dereva aliyevunja sheria anataka rushwa?” alisikika shuhuda mmoja akihoji kwa jazba.
Hata hivyo, pamoja na mkwara wa jamaa huyo, gari lake lilifanikiwa kuvutwa kuelekea polisi ambapo jamaa huyo alipanda gari lingine kulifuata.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate