HATIMAYE gazeti namba moja kwa habari za uchunguzi
Tanzania, Uwazi limeyanasa majina 403 ya Watanzania waliokamatwa,
kufungwa au kushikiliwa katika magereza mbalimbali duniani kwa makosa ya
madawa ya kulevya ‘unga’.
Baadhi ya watuhumuiwa waliokamatwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’.
Hivi karibuni, serikali ilikiri kukamatwa kwa Wabongo hao nje ya nchi
na kusema baadhi yao wanasubiri kunyongwa baada ya kupatikana na hatia.
Hata hivyo, serikali ilificha majina ya watu hao.
Ifuatayo ni orodha ya majina hayo na maeneo wanayotoka nchini Tanzania. Kwenye mabano ni hukumu zao.
Abdallah Ally Rashid Mbonde Fredue, Dar (miaka 15 jela), Mzia David
Michael, Dar (22), Rashid Mzonge, Magomeni, Dar (maisha), Salum Jumbe
Pigigi (maisha), Ramadhan Iddi Juma, Kinondoni, Dar (7), Saleh Happy
Hambona, Dar (18), Michael Dalasi Taraja, Temeke, Dar (19) na Juma Omar
Mgeni (kunyongwa).
Wengine ni Masumbuko Salum Hassan, Dar
(kunyongwa), Luka Joseph Urio, Dar (maisha), Masome Frorian Anthony, Dar
(maisha), Salum Mohammed Kitupura, Dar (kunyongwa), Begge Hemed Ahmed,
Tanga (15) na Mwanjati James Simon, Dar (maisha).
Wengine ni Mohammed Musa Mohammed, Dar (maisha), Omalla Donald
Nyowino, Dar (15), Yahya Ally Seif, Kinondoni, Dar (maisha), Chande
Mohammed Chande, Kinondoni, Dar (maisha), John James Amandus, Kinondoni,
Dar (kunyongwa), Bantulaki Isihaka Ally, Tanga (kunyongwa), Zungiza
Mohamed Ally, Dar (kunyongwa), Rashid Bakari Mzonge, Kimara Suka, Dar
(maisha), Mende Katija Mikidadi, Ilala, Dar (maisha), Shame Shame Udai,
Dar (maisha) na Mlenzi Mangala Hamisi, Dar (maisha).
Farida Sarboko Makarani, Zanzibar (kunyongwa), Adam Hariri Mohammed,
Magomeni, Dar (18), Said Mfaume Said, hajatajwa wa wapi (kunyongwa),
Mohammed Bakari Mkemi, haijatajwa wa wapi (kunyongwa), Mariam Ramadhan
Mahimbo, hajatajwa wa wapi (kunyongwa), Julieth Jonathan Jaspher,
haikusemwa anakotoka (kunyongwa), Halifa Matumla Ally, haijaandikwa
atokako (kunyongwa), Rajabu Salum Mwanyenza, haijaandikwa atokako
(kunyongwa), Ismail Mohammed Rajabu Mapusa, Magomeni Dar (maisha) na
Hamisi Kombo Ally (kunyongwa).
...hawa ni watuhumiwa wengine waliohusika .
Waliopo mbaroni ambao pia hawajaandikwa watokako ni: Sephu
Abdulrahman, Alfredy Thomas Singini, Lawrence Mbogoni Oni, Mohammed
Ibrahimu Kilima, Wilfred Casmir Mushi, Shakira Ahmed Mumba, Jackline
Benedict, Rajabu Rashidi Mshare, John Peter Martin, Abdallah Mwalimu
Mbaruk, Rashid Mzee Mrisho, Juma Ismail Nayopa, Tsakiris Costa Achelis
na Faith Michael Kabambe.
Wengine waliohukumiwa ni Bakari Badi Omari Mneko, Sinza, Dar (17),
Masomi Thomas Joseph, Dar (17), Abdallah Iddi Ally, Tabata, Dar (17),
Kondo Ally Mohammed (20), Mohammed Abubakar Nazzir (24), Abdallah Anwar
Abasi (24), Makuti Al- Jaribu Hassan, Kilwa, Lindi (25), Abdallah Iddi
Athuman (24), Mnyamani Hamad Ally, Tanga (22), Mtalu Rajabu Ally Rajabu,
Kariakoo, Dar (17) na Shughuli Kibaya Bakari, Tanga (8).
Wengine
ni Mfaume Omar Ng’anzi Msuya, Kariakoo, Dar (21), Steven Robert Onay
(9), Omar Juma Mang’enge (8), Steven Simon Kanul, Dar (8), Iddi Haji
Fumo, Unguja (9) na Seleman Hamisi, Unguja (8).
Pia wapo Athuman
Hassan Nash, Magomeni, Dar (8), Seleman Hussein Msimbe (8), Abdallah
Farid Twalib, Dar (17), Salim Ally Amani, haikutajwa anakotoka (22),
Calist Wilson Mosha, Arusha (18) na Saleh Abdul Omar, Kigogo, Dar (21).
Wengine ni Bugingo Sweetbert Rwezaura, Kijitonyama, Dar (21),
Mohammed Omari Ally, Zanzibar (19), Sayula Rashid Paul, hajatajwa
atokako (16), Koshuma Geofrey Gabriel, Kijitonyama, Dar (30) na Salim
Mrisho Hussein, Tanga (21).
Orodha inaendelea kama ifuatavyo: Riziki
Riziki Hamduni, Kinondoni, Dar (19), Bashir Rajabu Kafune, Magomeni,
Dar (19), Kharim Mohammed Omar, Ilala, Dar (19), Abubakar Abdul
Ligalwike, Kinondoni, Dar (8).
Wengine
waliofungwa na miaka yao katika mabano ni Pendo Ernest Kessy, Ilala,
Dar (9), Anna Kiula, Kijitonyama, Dar (9), Nuru Shebe Maftah,
Mwananyamala, Dar (9), Fatma Rashid, Dar (9) na Naima Abdulhafidh
Rashid, Mwananyamala, Dar (9).
Pia wapo Mariam Madaresa, Arusha na Dar (9), Mohammed Omar Ally,
Wete, Zanzibar (19), Faidhi Mohammed Abdallah, Kijitonyama, Dar (14),
Mohammed Ijumaa Rashid, Mbezi Beach, Dar (10), Omari Musa Abdallah,
Tanga (10), Zahra Ayubu Mwila, Korogwe na Kibaha (25) na Shamsa Gulum
Shambe, Magomeni Mwembechai, Dar (16).
Wengine
waliopo mbaroni ni Jeniffer Kessy, Mwananyamala, Dar, Shadia Issa,
Mbezi Beach, Dar, Rosemary Asakwe Kionaumela, Mapipa, Dar na Samir
Sandra Khalid.
Orodha ya waliohukumiwa inaendelea: Tatiana Bakari Chambo, Temeke,
Dar (11), Ramadhan Maneno Mtumwa, Kijitonyama, Dar (14), Yusuf Herold
John, Magomeni (18), Hassan Hiza Sebudu, Tanga (22), Halfa Abdallah
Ng’anga, Ilala, Dar (19) na Nelson Anthony Dhinner, Kigogo, Dar (14).
Wengine
waliohukumiwa ni Awadh Salehe Awadh, Kinondoni, Dar (24), Hasim Paul
Syula, Mapipa, Dar (16), Fussy Abdu Mussa, haijatajwa anakotokea (17),
Mtwanzi Carlos Adam, haijatwaja anakotoka (17) na Yusuf Abbas Kilima,
Dar (5).
Wafuatao wametiwa mbaroni; Salum Mhibu Mkwawira, Tunduma, Mbeya, Juma
Musa Juma wa Zanzibar, Nassor Mohammed Ayub wa Tanga, Jimmy Joseph
Kivelege wa Dar, Kilugage Joram Masembo wa Kahama, Shinyanga, Manengelo
Abdurahman wa Dar na Hamud Ali Mohammed (mji haukutajwa).
Wengine ni
Eric Charles Mkude wa Tanga, Makame Khatibu Ali wa Kiembesamaki,
Zanzibar, Abdulwahid Hamisi Mashauzi wa Singida, Said Ally Makame wa
Zanzibar, Peter George Gyellah wa Tegeta, Dar, Said Abdallah Mzee wa Dar
na Yusuf Chombo Khalid wa Dar.
Baadhi ya watuhumuiwa wa kike waliokamatwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ‘unga’.
Wafuatao wamehukumiwa na miaka yao kwenye mabano; Salehe Mohammed
Aboubakar, Tanga (20), Abdul Omar Salehe, Dar (14), Omari Hussein Ally,
Tanga (14), Kaliro Samson Majani Busagaga, Tarime, Mara (9), Mohammed
Salum Mbaraka, Moshi, Kilimanjaro (9), Zuberi Musa Zuberi, Zanzibar na
Dar (9), Adam Athumani Udindo (alikataa kutaja anakotoka, 14).
Wafuatao pia wapo mahabusu katika nchui mbalimbali, kesi zinaendelea;
Frank Thomas Frank (Moshi), Nasra Hassani Masogoa (Dar), Nice Saidi
Mbwana (Tanga na Dar), Josephine Raymond Malibanga (hakutaja atokako),
Sara Yuga Mtinda (Singida), Amina Khamisi Bwanga (hakutaja atokako),
Flora Frederick Siyame (Dar) na Zawadi Aloyce Henjewele (Songea).
Wengine ni Upendo Eric Shayo wa Moshi, Mariam Haruna Feruzi (Dar),
Yusta Riwa (Moshi Kilimanjaro), Watende Sudi Kiwamba (Tabora), Elizabeth
Yoram Kwambaza (Korogwe, Tanga), Mariam Shabibi (Dar) na Zahoro
Mohammed Nassoro (Tanga).
Wengine waliokamatwa na wako mahabusu ni Rashid Nassoro Maumba
(Mpanda), Mohamed Said Mrisho (Tanga), Suleiman Said Mpetula (Dar),
Shaban Salum Mnyimani (Dar), Abood Yasser Ali (Tanga), Juma Shabani
Ngoma (Tanga), Juma Akida Yusufu (Tanga) na Miraji Yusufu Semahimbo
(Tanga).
Wengine ni James Christopher Lukio (Tanga na Dar), Rabin Issa Mbaba
(Mafia), Abdallah Rajabu Dole (Dar), James Sakaya Henry (Dar), Bakari
Kheri Nassoro (Dar), Faraji Juma Lota (Dar), Gervas Anselm Muganda
Matura (Musoma), Rawe Waikama Magarya (Tarime) na Abdulraheem Sadiki
Mohamed (Dar).
Wafuatao wamehukumiwa na miaka yao kwenye mabano ila miji waliyotoka
Bongo haikutajwa; Rashid Habib Muhsin (9), Abdallah Saidi (16), Hiridi
Mamdadi Issa (12), Juma Mohammed Mapande (16), Mwatadi Kulwa Hamisi
(16), Hamisi Abdallah Mohammed (9), Erick John Ibrahim (16) na Abdallah
Farid Salum (9).
Thuweni Hamadi Suleiman, Kileo Walter Exaudy na Jacqueline Clifford Fitzpatricque (Jack Patrick) hawa bado hawajahukumiwa.
IDADI YA NCHI
Katika orodha hiyo, China wapo
Wabongo 65, Brazil 108, Kenya 34, Hong Kong 118, Pakistan 16, Falme za
Kiarabu 12, Japan 7, Morihsaz 6, Uingereza 5, Malawi 5, Uganda 4, Oman
3, Uswisi 2, Italia 2, Marekani 2, Argentina 2, Uturuki 1, Ureno 1,
Botswana 5, Chile 1, Afrika Kusini 3 na Msumbiji 1.
Orodha ni ndefu, kama una ndugu na unahisi amekumbwa na sakata hii
lakini jina lake halipo gazetini unaweza kufika Ofisi za Global
Publishers, Bamaga-Mwenge ukaoneshwa majina zaidi.
Uwazi liliongea na Kaimu Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa
Dawa za Kulevya, Aida Tesha (pichani) kuhusu kukamatwa kwa watu hao
ambapo alikiri na kusema kuwa serikali inaendelea kufuatilia takwimu za
Watanzania wengine ambao wamekamatwa nje ya nchi.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment