EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, July 15, 2014

MKE WA MTU ACHANJWA NYEMBE KISA FUMANIZI

CHANZO GLOBAL PUBLISHERS
MWANAMKE mmoja,  Rehema Juma (21) ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Mtaa wa Msamvu B, Kata ya Kihonda Maghorofani mkoani Morogoro amechanwa na nyembe mwilini na baadaye kutembezwa bila nguo mtaani mchana kweupe akituhumiwa kufumwa na mume wa mtu.
...Aliyekatwa nyembe.
Tukio hilo la aina yake  ambalo lilivuta umati mkubwa, lilitokea Julai 5, mwaka huu saa 10 jioni katika Mtaa wa Msamvu B.
Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mwandishi wetu walidai kuwa kwa muda mrefu, Zaitun Ally (30) ambaye pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu Rehema akidai anatembea na mumewe, hivyo akaamua kutega mtego bila mafanikio.

“Zaituni baada ya kushindwa kuwanasa leo aliamua kumuita Rehema nyumbani kwake na kudai amewafuma na mumewe hivyo kumchana nyembe baadaye kumvua nguo na kumtembeza bila nguo mtaani hadi nyumbani kwake umbali wa mita 300 mchana kweupe,” alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Ashura Ally.
Rehema Juma akiwa na mama yake.
Mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Rehema na kumkuta akiwa amefungwa bendeji sehemu za mwili wake na alipoulizwa alifafanua:
“Ni kweli tukio hilo limetokea lakini siwezi kuzunguma peke yangu, twende kwa mama mkwe Mtaa wa Ngerengere.”
Mwandishi wetu na Rehema walipofika kwa mkwe wa mtuhumiwa, Lilian Julius Sechonge ambaye ni mjumbe wa serikali za mtaa wa Ngerengere na kutakiwa kuzungumzia tukio hilo alikuwa na haya ya kusema:
Mtuhumiwa wa tukio hilo.
“Ni kweli Rehema ni mkwe wangu kwa mwanangu aitwaye Godfrey Sechonge anayeishi naye hadi sasa, Julai 5, mwaka huu mwanangu huyo alikuja na akaniambia mkewe anatembezwa bila nguo.
“Nilifika eneo la tukio na kumkuta mkwe wangu yuko uchi huku akivuja damu mwili mzima.
“Aliniambia amecharangwa viwembe na Zaituni akimshutumu kutembea na mumewe, nilimchukua mwanangu na kumkimbiza polisi ambapo tulipewa PF3 na kufunguliwa jalada namba MOR/RB/4009/2014.”
Naye Rehema alipozungumzia kisa hicho alisema siku ya tukio saa 4 asubuhi, Zaituni alimtuma mwanaye nyumbani kwake na kumuomba aende kwake (Zaituni).
“Nilipofika kwake aliniingiza ndani na kuniwekea kisu shingoni huku mwanaye akinirekodi na simu yake, akaniuliza nimetembea mara ngapi na mumewe!
“Alitaka kujua pia amenihonga shilingi ngapi, kwa hofu ya kuchinjwa nilikubali kwamba nilitembea naye mara moja na alinipa shilingi elfu tano. “Baada ya kusema hivyo akaniachia, nikarudi nyumbani.
Saa kumi aliniita tena, nilipofika nikamkuta yuko na mumewe na watoto wao, akaniuliza unamjua huyu? Nikamwambia simjui, akatoa simu na kufungua mahojiano, mumewe alipojaribu kumpora, akamchanja na wembe.
Mtuhumiwa akihojiwa.
“Ghafla akahamia kwangu na kuanza kunichanja kwa wembe huku nikipiga kelele na akanivua nguo kisha akanitoa nje na kunipeleka kwangu nikiwa na nguo ya ndani tu,” alisema Rehama.              
Akizungumza na mwandishi wetu diwani wa kata hiyo, Lydia Mbihaji alisema tangu aanze kuongoza watu hajawahi kukutana na tukio kama hilo ambalo aliliita ni la kinyama.
Tayari Rehema amelifikisha sakata hilo polisi na Zaituni alikamatwa na kuwekewa dhamana na mumewe akisubiri kuburuzwa mahakamani wakati wowote.
Baada ya kudhaminiwa, mwandishi wetu aliwashuhudia Zaituni na mumewe wakizungumza na Rehema ambapo inadaiwa wanataka ipatikane suluhu kabla kesi haijaanza kuunguruma mahakamani.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate