EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, July 26, 2014

MWANAUME AZAMISHWA SHOKA KICHWANI


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
NI tukio la kutisha! Tukio hilo linadaiwa kutokea jijini Mwanza ambapo mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja) amepigwa shoka la upande wa kushoto wa kchwa na kuzama ndani ikidaiwa ni sababu ya kufumaniwa.

Mgonjwa akiwa wodini na shoka kichwani.
Picha za tukio hilo zilitumbukizwa mitandaoni na mtu anayedaiwa ni daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji mtuhumiwa huyo.

TAARIFA FUPI
Kwenye mitandao ya kijamii, picha hizo ziliambatana na maelezo mafupi sana kwa chini yakisomeka hivi:

“Baada ya madoctor (madaktari) wa Bugando kupambana kuokoa maisha ya jamaa aliyefumaniwa huko Mwanza hatimaye wamefanikiwa kumtoa shoka kichwani na hali yake bado mbaya, yuko ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) kwa uangalizi zaidi. Mke wa mtu sumu!”
MAZINGIRA YA PICHA
Kwenye baadhi ya picha, mwanaume huyo anaonekana ana nywele ndefu kidogo na mustachi ulionona. Picha nyingine zinamuonea akiwa na kipara nusu kichwa baada ya kunyolewa nywele ili madaktari waweze kumfanyia upasuaji wa kulitoa shoka hilo lililozama ndani sana.

MAZINGIRA YA HOSPITALI
Baadhi ya watu waliochangia kwenye mitandao ya kijamii walisema tukio hilo lilitokea nje ya Tanzania. Walisema ingekuwa Bongo lazima vyombo vya habari vingeandika lakini hata hivyo, mazingira ya chumba cha upasuaji alicholazwa mwanaume huyo yalionesha ni Tanzania.

Shoka likiwa limetolewa na madaktari wa upasuaji.
KWA NINI NI TANZANIA?
Ni Tanzania kwa sababu, picha zinamuonesha mwanaume huyo akiwa kwenye kitanda cha chumba cha upasuaji akiwa amefunikwa shuka yenye maandishi yanayosomeka kwa kifupi MSD.
MSD ni kifupi cha maneno Medical Stores Department (Bohari Kuu ya Dawa). Mbali na kugawa dawa katika hospitali za serikali nchini, pia MSD inatoa mashuka yenye nembo hiyo kwa ajli ya kujifunika wagonjwa mahospitalini.

RPC ASHTUKA
Ili kupata ukweli wa madai hayo kwamba mwanaume huyo alikutwa na mkasa huo mkoani Mwanza na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Risasi Jumamosi liliingia kazini kufuatilia tukio hilo kwa kuzungumza na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime na kumuuliza kama ana ishu hiyo mezani kwake.

“Mh! Hivi nyiye mnajua kama mitandao siku hizi imezua balaa kubwa sana? Hivi tukio kama hilo, mwanaume apigwe shoka mpaka kuzama kichwani, alazwe Bugando Hospital mimi nisijue?
“Hakuna kitu kama hicho.

Hayo ni mambo ya mitandao tu, sijui wametoa wapi? Halafu si umeona hata maelezo hayajitoshelezi? Mimi mkoa wangu upo shwari kabisa mpaka hivi ninavyoongea na wewe,” alisema Afande Fuime kwa sauti iliyoashiria kushtuka.
Picha ya X-Ray shoka lilivyoingia pichani.
DAKTARI BUGANDO AONGEA
Ili kuchimba zaidi, Risasi Jumamosi lilimtuma paparazi wake aliye Mwanza, Mashaka Bartazal ambaye alikwenda hadi Hospitali ya Rufaa, Bugando na kuzungumza na daktari mmoja anayefanya kazi kwenye kitengo cha upasuaji ambapo alisema:

“Ni kweli tunapokea watu wenye matukio ya kutisha lakini mwanaume aliyepigwa shoka mpaka likazama kichwani hatujampokea,” alisema daktari huyo akiomba asitajwe jina gazetini kwani si msemaji wa hospitali hiyo. 
UKIO LAHAMISHIWA KAHAMA
Katika hali iliyozidi kuibua maswali, baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi wetu wa Mwanza walisema wamesikia mwanaume huyo alikumbwa na balaa hilo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

RISASI JUMAMOSI KAHAMA
Kwa sababu Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa Bongo ina waandishi nchi nzima, ilimwagiza mwandishi wake aishiye Kahama kulisaka tukio hilo na kutoa ripoti Makao Makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar ambapo alifanya hivyo kwa kuomba apewe saa mbili tu kufuatilia.

Baada ya saa mbili kupita, mwandishi wetu alitoa ripoti makao makuu kwamba, hakuna mwanaume aliyelazwa kwenye hospitali yoyote ya wilayani Kahama wala mkoa huo kwa kupigwa shoka la kichwani.
MASWALI YA MSINGI
Bado jamii imebaki na maswali kadhaa ya kujiuliza. Kwamba, kama ni tukio la Tanzania, hiyo sehemu aliyolazwa mtu huyo hakuna jeshi la polisi? Kwa sababu polisi ndiyo wanahusika na kupewa taarifa za matukio kama hayo na kuyatangaza.

Pili, jamii inauliza kwamba, inawezekana mwanaume huyo baada ya tukio hakupitia au kupitishwa polisi kwa ajili ya kupewa Police Form No. 3 (PF3)?
Kama ni hivyo, hospitali walimpokeaje mtu wa hivyo hasa ikizingatiwa kuwa, hali yake ilionekana ni mbaya kwani hata picha ya X-Ray ilionesha shoka hilo lilizama kiasi cha kama inchi sita kwenda ndani na kubakiza kidogo kutokea upande wa kulia wa kichwa.
UKWELI BADO UNATAFUTWA
Bado Magazeti Pendwa ya Global Publishers (Uwazi, Risasi, Ijumaa, Amani na Ijumaa Wikienda) yanaendelea kuchimba tukio hilo ambalo limeonekana kuishtua sana jamii.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate