Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge
amewataka wananchi kupuuza taarifa zozote zinazotolewa kwa jina lake
kupitia mtandao wa facebook kwa kuwa yeye hatumii mtandao huo.
Waziri Mahenge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete mkoani
Njombe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wetu wilayani
hapo na kusema kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mitandao hiyo
vibaya kwa kufungua akaunti yenye jina lake ilihali yeye hajawahi
kujiunga na facebook na hana mpango huo.
Amesema kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali wapo watu
wanaoziamini taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia mtandao huo
wakidhani zimetolewa na yeye lakini imekuwa tofauti na kuwataka wananchi
kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa zinatolewa na mtu ama watu fulani na si
yeye.
"Ukiangalia pale pana picha yangu kweli, lakini taarifa zingine ni
uongo mtupu, kwa mfano tarehe yangu ya kuzaliwa iliyoandikwa hapo sia
ya kweli, hii inaashiria wanavyoviweka ni vya uongo" amesema Waziri
Mahenge.
Aidha ametoa rai watu kuitumia vizuri mitandao hiyo kwa kuisaidia
jamii huku akiwataka waliofungua akaunti hiyo kuifunga na kuacha
kuwapotosha watu kwa kutumia jina lake kwani ni kinyume cha sheria na
atakayebainika sheria iko wazi dhidi yake.
Hivi karibuni kumekuwa na watu fulani kufungua akaunti kwnye
mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya viongozi mbalimbali kwa lengo
la kuwahadaa watu na kuwapa taarigfa ambazo si sahihi
Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete
No comments:
Post a Comment