MWANAFUNZI
wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Vena Mtati
(27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai
mazito ya kumuua mtoto wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa
rambo na kuutia ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha chini ya
kitanda, Uwazi lina habari ya motomoto!
Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa
kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi,
lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni,
Kata ya Mvinjeni mjini hapa.
SHUHUDA
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito.
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito.
“Wiki mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce
ambaye alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba
kubwa, baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Siku ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji alitoka
kwenda katika shughuli zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani
ndipo aliposhikwa na uchungu, akajifugua mtoto wa kike.
“Ilikuwa asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.
“Ilikuwa asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.
“Tuliposikiliza kwa makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili
kufanya kelele hizo zisisikike kwa nje. Lakini kwa vile sisi majirani
tulijua kwamba ndani ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga
mtoto si za kawaida ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),”
kilisema chanzo hicho.
HATUA ZA HARAKA
Mwandishi wetu alipopatikana na kunyetishiwa kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa mama ambaye ni nesi kumuua mtoto wake aliyejifungua, aliwasiliana na Polisi wa Dawati la Jinsia.
Mwandishi wetu alipopatikana na kunyetishiwa kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa mama ambaye ni nesi kumuua mtoto wake aliyejifungua, aliwasiliana na Polisi wa Dawati la Jinsia.
Polisi hao, awali walimtafuta mwenyeji wa mtuhumiwa huyo, yaani Joyce
ambaye alikuwa kwenye mihangaiko yake. Alipopatikana alipokonywa simu
yake ya mkononi ili asiweze kuwasiliana na mtuhumiwa.
Aliulizwa kama ana mgeni nyumbani kwake, akakiri. Akaulizwa kama
mgeni huyo amejifungua, akakataa ndipo wakamchukua kwenda naye nyumbani
kwake kumfuata mtuhumiwa huyo.
ASKARI WAFIKA ENEO LA TUKIO
Paparazi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Paparazi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Alipoulizwa kama amejifungua, awali alikataa katakata lakini baada
ya kubanwa na kutishiwa kuswekwa ndani, alikiri kujifungua na kusema
kwamba mtoto huyo amemficha uvunguni mwa kitanda.
Denti (aliyeshika kiroba chenye mwili) akiwa chini ya ulinzi wa polisi (Kulia) ni mwenyeji wake, Joyce.
DAMU SAKAFUNI
Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati akijifungua mwenyewe!
Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati akijifungua mwenyewe!
POLISI WAPEKUA UVUNGUNI
Polisi walizama chumbani, wakainama kuchungulia chini ya kitanda. Walichoanza kukiona ni mfuko wa salfeti, wakauvuta kuutoa. Walipofungua ndani, wakakuta mfuko wa rambo, wakaingiza mkono na kutoa kifurushi kikiwa kimeviringishwa nguo nyingi na ndiye mtoto huyo alimohifadhiwa.

HEBU SOMA HII, INAUMA ZAIDI
Mbali na mwili wa mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia ulimwagiwa chumvi na vumbi la mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili mwili huo usitoe harufu utakapotupwa porini.
Mbali na mwili wa mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia ulimwagiwa chumvi na vumbi la mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili mwili huo usitoe harufu utakapotupwa porini.
Majirani walisema maarifa hayo, mtuhumiwa aliyapata kwa sababu tayari
anajua namna ya kuhifadhi mwili wa mwanadamu, kwa mwanamke asiye na
ujuzi asingeweza kufanya hivyo.
SABABU YA MTOTO KUUAWA
Kuna madai kwamba, mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito aishiye jijini Dar es Salaam kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini.
Kuna madai kwamba, mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito aishiye jijini Dar es Salaam kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini.
ORODHA YA WALIOKAMATWA
Baada ya polisi kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo, walimkamata yeye, mwenyeji wake Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana mara moja.
Baada ya polisi kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo, walimkamata yeye, mwenyeji wake Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana mara moja.
Polisi walisema mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa kwa sababu alikiuka
sheria za mji ambapo alitakiwa kutoa taarifa za kumpokea mgeni huyo
kwenye serikali za mitaa lakini hakufanya hivyo huku Joyce akidaiwa
kutambua kuwa mgeni wake alijifungua lakini akawaambia hakujifungua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment