EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 27, 2014

MHE. LIBERATA MULAMULA AKUTANA NA MHE. ARNELL MILLS, MEYA WA MJI WA HELENA-WEST HELENA KUTOKA JIMBO LA ARKANSAS MAREKANI‏


Mhe. Meya Wills akipokelewa na Bw.Suleiman Saleh, Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Washington DC mara baada ya kuwasili Ubalozini hapo kwa mazungumzo na Mhe. Balozi Liberata Mulamula

Mhe. Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika mazungumzo na Mhe.Arnell Wills, Meya wa mji wa Helena-West Helena, Arkansas, Marekani,Ubalozini Tanzania House, Washington DC.
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Meya Wills zawadi maalum kutoka Ubalozini.
.Mhe. Mulamula akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya Wills wa Mji wa Helena –West Helena, Arkansas, Marekani. 

Balozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula jana Jumanne Agosti 26, 2014, alikutana na Mhe. Mstahiki Meya wa Mji wa Helena-West Helena kutoka jimbo la Arkansas, Marekani, Ubalozini “Tanzania House” Washington DC. Mhe. Wills ambaye  Mji wake wake wa  Helena-West Helena una mahusiano ya kidada (Sister City) na Mji wa Moshi, Tanzania, alifika Ubalozini ili kufahamiana na Mhe.Balozi Mulamula pamoja na kumuelezea mashirikiano yaliyopo baina ya Mji wa Helena-West Helena na Moshi ambapo makubaliano rasmi yalisainiwa Oktoba 12, 2012, hapa Marekani kufuatia ziara ya Mhe. Japhary Michael, Meya wa Mji wa Moshi katika mji wa Helena –West Helena, Arkansas.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Wills alimuelezea Mhe. Balozi Mulamula juhudi zake katika kuimarisha mashirikiano hayo ya miji hiyo miwili ambapo yamejikita zaidi katika sekta ya utalii pamoja na shughuli nyingine za kukuza uchumi. Balozi Mulamula alimshukuru Meya Wills kwa kumtembelea na kufurahishwa na Meya huyo kutokana na kutembelea Tanzania mara mbili na kupata ufahamu zaidi wa Tanzania na hivyo kusaidia kupanua mahusiano yaliyopo baina ya Moshi na Helena –West Helena. Mhe. Mulamula alimshauri Mhe. Meya Wills kupanua wigo wa ushirikiano huo katika sekta nyingine za uchumi, biashara na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate