WATANI
wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba SC na Yanga watakutana Oktoba
12, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ladha
ya Ligi Kuu ni mechi baina ya miamba hiyo miwili nchini- na kidogo
mechi zinazozihusisha timu hizo na mabingwa watetezi, Azam FC, nazo pia
huwa za kukata na shoka.
Msimu
uliopita, mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 3-3, Simba
wakitoka nyuma kwa 3-0 hadi mapumziko na marudiano, Yanga walisawazisha
dakika za lala salama kupata sare ya 1-1.
Kocha Patrick Phiri wa Simba SC atakutana na watani Yanga SC, Oktoba 12 mwaka huu Uwanja wa Taifa |
Lakini
Simba SC ilijichukulia ubabe wa jumla wa msimu dhidi ya watani wao,
baada ya kuwafunga Yanga SC 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe
Desemba mwaka jana Uwanja wa Taifa.
Mzunguko wa pili, timu hizo zitakutana Februari 8, mwakani, mchezo wa kwanza Yanga mwenyeji, wa pili Simba mwenyeji.
Azam FC na Simba zitakutana Januari 1, mwaka 2015 wakati marudiano yatakuwa ni Aprili 12, mwaka huo.
No comments:
Post a Comment