EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, August 16, 2014

TANZANIA MWENYEJI WA MASHINDANO YA 8 YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI


Mkuu wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya Majeshi Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkuta huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo tofauti wakimsikiliza Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman (hayupo pichani) katika Mkutano wake na wandishi.

Mkurugenzi wa ufundi wa mashindano hayo Luteni  Kanali Joseph Bakari akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Michezo ya nane ya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 18 mwezi  huu.
Akitoa Taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  Makao Mkuu ya Brigedi Migombani kwa waandishi wa Habari, Mkuu wa Brigedi hiyo Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman amesema lengo la michezo hiyo  ni kujenga  mashirikiano kati ya Majeshi na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema katika Michezo hiyo kutakuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa na wote watakuwa washindi, lengo ni kujenga uweledi na nidhamu ndani ya majeshi yetu.
“Hii ni fursa ya wanajeshi wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana pamoja kama tunavyofanya katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi”, alisema Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman.
Amezitaja Nchi za Jumuiya hiyo zitakazoshiriki  Michezo hiyo kuwa ni wenyeji Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya  na Uganda.  Amesema Michezo itakayochezwa na wanajeshi hao ni  Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu  na Mbio za nyika  na ameelezea viwanja vitakavyofanyika kwa ajili ya michezo hiyo  Polisi ziwani ,Vyuo vya Mfunzo Kilimani, JKU Saateni, Pamoja na Viwanja vya Zimamoto na Uokozi.
Brigedia Jenerali Sharif Sheikh ambaye pia ni Makamo  Mwenyekiti wa Michezo hiyo, amewataka  Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuona vipaji vitakavyoonyeshwa na wanajeshi kutoka Nchi hizo .
Akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo Leftinenti Kanali Joseph Bakari amesema pamoja na micheo hiyo kutakuwa na Burudani ya Ngoma za Utamaduni kutoka Vikosi vya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema jumla ya wanamichezo 505 wakiwemo Viongozi kutoka Nchi hizo watashiriki michezo hiyo itakayodumu kwa muda ya wiki mbili.  
Na Miza Othman Makame   Maelezo- Zanzibar .

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate