EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 13, 2014

VAN PERSIE ANATESA NA MAUZO YA JEZI ENGLAND, BONGO HAINA MWENYEWE
Na Saleh Ally
UMESIKIA taarifa za England kuhusiana na mauzo ya jezi? Mshambuliaji nyota wa Manchester United ndiye aliyemaliza msimu akiongoza kwa mauzo.
Jezi yake namba 20, ndiyo iliyouzwa zaidi kuliko nyingine ikiwa ni msimu mmoja tu baada ya kujiunga na Mashetani Wekundu akitokea Arsenal.
Mholanzi huyo amempiku mkongwe Steven Gerrard, nahodha wa Liverpool na kipenzi cha Waingereza wengi. Gerrard amepaa katika mauzo ya jezi kutokana na mwendo mzuri wa Liverpool katika msimu huo uliopita.

Baada ya Gerrard, fowadi Luis Suarez ameshika nafasi ya tatu akiwa na jezi namba 7 ya Liverpool, sasa ameiacha na kutua Barcelona.

Nafasi ya nne imekwenda kwa Eden Hazard wa Chelsea, halafu tano bora ikafungwa na Mesut Ozil aliyekuwa ametua Arsenal akitokea kwa vigogo, Real Madrid.
Wengine wanaofunga 10 bora ya jezi zinazouzwa zaidi katika Ligi Kuu England msimu uliopita ni Wayne Rooney (Manchester United), Sergio Aguero (Manchester City), Juan Mata (Manchester United), Shinji Kagawa (Manchester United) na Frank Lampard (Chelsea).
Hiyo ni 10 bora ya England, jiulize ya Tanzania Bara iko wapi, si rahisi kuwa na jibu wala kupata takwimu kwa kuwa klabu kubwa na zile maarufu za Tanzania wala hazijihusishi na biashara ya kuuza jezi.
Si kwamba haziamini hiyo ni biashara, lakini uvivu na kuridhika na viingilio vya milangoni na fedha kidogo za wadhamini, kwao inatosha.
Ukiangalia katika 10 bora ya England, utaona biashara imekuwa kubwa zaidi kwa wachezaji wanaosajiliwa kutoka klabu moja kwenda nyingine na wale wakongwe wanaokubalika sana kama Gerrard na Lampard, mauzo ya jezi zao yanaendelea kuwa juu.
Pia inategemea aina ya timu, kwani Fernando Torres alikaa kileleni kwa misimu mitatu mfululizo, wakati huo akiwa Liverpool, lakini baada ya kutua Chelsea, taratibu ameporomoka hadi kuondoka kabisa 10 bora.
Hapa nyumbani, Yanga na Simba ndiyo walikuwa na nafasi kubwa ya kufanya biashara kwa kutumia jezi za wachezaji fulani, halafu Mbeya City, Azam FC, Mtibwa Sugar na nyingine zingefuatia.
Angalia wakati wa usajili wa Emmanuel Okwi, Yanga wangeuza jezi kiasi gani na wangeingiza fedha kiasi kipi?
Hiyo haitoshi, usajili kwa ajili ya msimu ujao, Jaja, Coutinho, lazima wangeiingizia Yanga fedha nyingi kama ilivyo kwa Simba na Paul Kiongera, Pierre Kwizera, Amissi Tambwe na wengine.

Vipi sasa klabu hizo hazina hesabu ya kutengeneza fedha wakati kuna soko? Angalia Barcelona baada ya kukubaliana tu na Suarez, jezi zikaingia sokoni, mamilioni yakapatikana.
Klabu za Yanga, Simba na nyingine hazina wabunifu, watu hawaelewi au wavivu wa kazi. Basi wana kila sababu ya kujifunza, wakishindwa waombe ushauri.
10 YA JEZI ZINAZOUZA SANA ENGLAND:

1. Robin van Persie

2. Steven Gerrard

3. Luis Suarez

4. Eden Hazard

5. Mesut Ozil

6. Wayne Rooney

7. Sergio Aguero

8. Juan Mata

9. Shinji Kagawa

10. Frank Lampard10 BORA BONGO KAMA WANGEKUWA MAKINI:

1.     Coutinho

2.     Paul Kiongera

3.     Jaja

4.     Amissi Tambwe

5.     Mrisho Ngassa

6.     Shabani Kisiga

7.     Mwagane Yeya

8.     Kipre Tchetche

9.     Pierre Kwizera

10.  John Bocco

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate