EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 6, 2014

Warioba: Bunge litapoteza fedha za wananchi endapo hakuna maridhiano

 
Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo baada ya kuanza kwa vikao vyake mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman 
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema kuendelea vikao vya Bunge Maalumu la Katiba bila kuwapo maridhiano baina ya pande zinazovutana na upande mmoja ukibaki nje ya Bunge, ni sawa na kutumia vibaya fedha za Watanzania.
Amesema kauli kwamba akidi ya wajumbe wa Bunge hilo imetimia na vikao vinaweza kuendelea haiwezi kuzaa Katiba itakayokubaliwa na wananchi wote na ni tofauti na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyoeleza katika sehemu ya kufanya uamuzi.
Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wetu ofisini kwake Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema, “Kama uwezekano wa kukutana upo, kwa nini Bunge liendelee kutumia fedha wakati mnajua kuwa mwisho hamtafikia uamuzi? Jambo la msingi ni kujitahidi kuafikiana na Bunge liwe na wajumbe wote.”


Kauli ya Warioba imeungwa mkono na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba wakati akichangia hoja ya mabadiliko ya kanuni ya Bunge hilo kwa kulitaka bunge hilo kujitathimini iwapo baada ya mjadala litaweza kufikia uamuzi, ili kuepuka matumizi mabaya ya fedha za walipakodi.
Akitoa hadhari hiyo bungeni jana, Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, alisema ni vyema Bunge hilo likajiridhisha kuhusu namna linavyoweza kutumia siku 60 zilizowekwa kwa uhakika na umuhimu wa kuziondoa siku za Jumamosi kitendo kinachosababisha kuongezeka hadi kufikia 84.

“Tujiridhishe na kukubali ukweli kwamba kukaa hapa kwa siku 84 bila uhakika wa kupatikana kwa theluthi mbili kwa pande zote mbili inayohitajika kupitisha rasimu hii haiwezi kueleweka kwa Watanzania. Ni lazima Watanzania watatuuliza tumefanya nini,” alisema.
Alisema kwa namna moja, ni vyema kujua idadi halisi ya wale wanaoshiriki katika awamu ya pili ya Bunge hilo na wale wasioshiriki, ili kutoa uthibitisho wa kihesabu kwamba uamuzi wa kuendelea kwa bunge unaweza kuwa na maana.

Hata hivyo, Nchemba alisema ni vyema wakiendelea kujadili masuala muhimu na kwa kuwa wanakwenda kujadili sura muhimu zinazogusa moja kwa moja maisha ya Watanzania, lakini kwa uhakika kwamba hatua hiyo itakuwa na manufaa kwa Watanzania katika hatua ya mwisho.
Alisisitiza kwamba iwapo hatua hiyo itashindikana, utetezi wa mwisho hautaweza kueleweka kwa sababu suala la kutimia kwa akidi kwa mujibu wa Katiba ni muhimu katika kufikia uamuzi na hasa kuangalia upya umuhimu wa kufikia maridhiano kwa sasa.
Bunge la Katiba lilianza jana mjini Dodoma bila kuwapo kwa wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na baadhi ya wajumbe 201 wa kuteuliwa na Rais waliosusa vikao hivyo.
Ukawa wanashinikiza kujadiliwa kwa rasimu ya Katiba iliyotolewa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na si ile iliyodai inaingizwa kinyemela na wajumbe wanaounga msimamo wa CCM wa serikali mbili badala ya tatu zilizopendekezwa na rasimu.
Akizungumzia hali hiyo Jaji Warioba alisema: “Hatuwezi kupata Katiba ambayo itakubaliwa na Watanzania bila makundi yote kukubaliana. Ushauri wangu kwa makundi yanayovutana ni kufikia mwafaka na kwenda bungeni kufanya kazi kwa pamoja.”
Alisema kitendo cha upande mmoja kuendelea na vikao vya Bunge hilo bila upande mwingine kuwapo, hakina faida yoyote kwa sababu mwishoni hawataweza kuchukua uamuzi wowote.
“Hawawezi kufanya uamuzi wowote kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaeleza kuwa ili uamuzi ufanyike ni lazima iwepo theluthi mbili ya wajumbe kutoka kila upande wa muungano.
“Itakuwa na matatizo zaidi kama mkitunga Katiba na kuipitisha kwa idadi fulani ya watu na kuanza kupingwa wakati huohuo.”

Afafanua madai ya Lukuvi
Katika hatua nyingine, Jaji Joseph Warioba alifafanua madai yaliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kuwa yeye (Warioba) amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Alisema maoni hayo aliyoyawasilisha serikalini Machi 27, mwaka huu yalikuwa maoni yaliyotolewa na wananchi lakini hayakuingizwa katika Rasimu kwa kuwa yanahusu tu Tanganyika, kwa kuwa Rasimu iliyoandaliwa ilipendekeza serikali tatu na Zanzibar wana utaratibu wao.
“Tuliona kuwa sura hizo hazifai kuwa katika Katiba ya Jamhuri kwa sababu masuala hayo mawili; ardhi, Zanzibar wana sheria na utaratibu wao, Tanzania Bara wana sheria na utaratibu wake” alisema kama ilivyo wa Serikali za Mitaa.
CHANZO NI MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate