EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, August 23, 2014

WOLPER ALIA KUTOPATA MTOTO

SUPER lady kunako tasnia ya sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe (26), anadaiwa kuangua kilio kisa kutopata mtoto, Risasi Jumamosi limeinyaka.
Super lady kunako tasnia ya sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
KUMBE!
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wake wa karibu, staa huyo amekuwa akihaha kusaka mtoto huku shinikizo likitoka kwa bibi yake, mzaa baba ambaye amekuwa akimuuliza juu ya yeye kumpata mtoto kwani umri unazidi kuyoyoma.
MADAKTARI WANASEMAJE?
Habari zilidai kwamba mwanadashosti huyo alishakwenda kwa madaktari mbalimbali ambao walimtaka kutokuwa na pupa kuhusiana na suala hilo na zaidi azidi kumuomba Mungu.
CHANZO CHATIRIRIKA
“Unajua umri ukishasogea, wanawake wengi huwa na wasiwasi juu ya suala hilo la kupata mtoto kama ilivyo ishu ya kusaka ndoa maana ni kati ya vitu vinavyowatesa.
Jacqueline Wolper Massawe.
“Wolper ana wataalam wake lakini hawajamwambia kama ana tatizo la kutopata mtoto.
“Kuna maelekezo ambayo wamekuwa wakimpa ambayo humrejeshea furaha anapowaza ishu hiyo.”

HOFU TUPU!
“Madaktari walimwambia tatizo la kutopata ujauzito ina maana mwanaume na mwanamke au watu walio katika uhusiano wa kutafuta ujauzito ndani ya mwaka mmoja wameshajitahidi kufanya hivyo lakini wameshindwa.
“Walimwambia pia inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani kiwango cha chini ni mwaka mmoja ambacho Wolper alishakuwa na mwanaume lakini hakufanikiwa ndiyo maana wakati mwingine anakuwa na hofu.
“Kuna wengine wanamwogopesha wanapomwambia kukosa mtoto ni tatizo kubwa katika jamii kwani kila mwanamke  anataka afikie malengo ya kuwa na familia na hasa kunapokuwa na shinikizo la wazazi wanataka mjukuu. 
TATIZO LIPO UPANDE WA PILI?
“Katika maelezo yao, madaktari walimwambia si mwanamke pekee anayeweza kuwa na tatizo bali hata mwanaume, hivyo tatizo linaweza kuwa kwa hao wanaume aliowahi kuchepuka nao,” chanzo kilimaliza kutiririka huku kikiomba hifadhi ya jina hadi atakaporudi mwana wa Adamu.
WOLPER APATIKANA
Baada ya kujazwa data hizo, gazeti hili lilimsaka Wolper ambapo alipopatikana, alifunguka kila kitu juu ya ishu hiyo.
BIBI YAKE KAMUONGEZEA MACHUNGU?
Akizungumza na gazeti hili mara tu baada ya kutua Dar kwa ndege akitokea mkoani Kilimanjaro ambako alikwenda kumsalimia bibi yake huko Old Moshi, staa huyo alisema kwamba hakuna siku ambayo aliumia kama alivyokwenda kijijini na kukutana na bibi yake na kuanza kumuuliza kuhusu lini atapata mtoto.
“Kiukweli hakuna kitu ambacho kiliniingia kwenye moyo kama bibi yangu kuniuliza kuhusu mtoto, nimejikuta nikitoa machozi tu. Ni kama alitonesha kidonda,” alisema mdada huyo.
Wolper alisema kuwa bibi yake alimsisitiza kwamba asijali kuhusu mtoto atakula nini  bali akimpata ampeleke kwake kwani atakula chochote atakachokula bibi huyo.
Katika maelezo mengine, Wolper alisema amejitahidi sana kutafuta mtoto lakini imeshindikana lakini anamuamini Mungu kuwa atampata kulingana na matakwa yake.
“Nimejitahidi sana kusaka mtoto lakini imeshindikana hivyo kwa wale ambao wanabahatika kupata mimba nawashauri wasitoe maana mtoto ni faraja kubwa kwa wanawake,” alisema Wolper.
CHANGAMOTO KUMPATA BABA BORA
Wolper aliongeza kwamba aliyachukua maneno ya bibi yake kwa mikono miwili na atayafanyia kazi, inawezakana mpaka mwakani anaweza kulikamilisha hilo lakini kuna changamoto moja tu anayokumbana nayo nayi ni  nani wa kuzaa naye ambaye atakuwa baba bora wa mwanaye.
“Unajua unaweza kuzaa mtoto wala isiwe tabu kumlea kabisa kwani wapo watu wengi wanaweza kumwangalia, tatizo ni nani wa kuzaa naye tu jamani,” alisema Wolper huku akiamini kuwa siku ikifika Mungu atamjalia mtoto.
WALISHINDWA KUZAA NAYE?
Wolper aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na wanaume kadhaa wakiwemo mastaa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Khalid Juma ‘Jux’ na yule mwanaume aliyezua naye tafrani kabla ya kumwagana, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ na huyu wa sasa ambaye bado hajamuanika jina, wote eti wameshindwa kuzaa naye.
CHANZO NI GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate