EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 4, 2014

BABA ALIVYOMNYONGA MWANAYE NA KUMZIKA

Na Mwandishi Wetu, Katavi YULE mtoto wa umri  wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey aliyeuawa kikatili kwa kunyongwa kisha kuzikwa na baba yake mzazi, Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’ (27) kwa kuwa alizaliwa akiwa ametanguliza makalio yake, amezidi kuibua maswali.
Mtuhumiwa Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’( katikati) aliyemuua mwanaye mwenye umri  wa mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey.

Baadhi ya wakazi wa Katavi waliozungumza na gazeti hili juzi, walihoji uhalali wa baba kumjadili mtoto katika kuzaliwa kwa sababu ya kutanguliza kiungo fulani.
Wengine walitaka kujua ni kwa nini kama kumuua mtoto wake, mzazi huyo alisubiri kwa mwaka mmoja na miezi miwili?
Mtuhumiwa ambaye pia ni mganga wa kienyeji anayeishi Kitongoji cha Mwikang’ombe, Kijiji cha Katuma wilayani Mpanda, alitenda unyama huo  kwa madai kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa ametanguliza makalio, hivyo ni nuksi kubwa katika shughuli zake za uganga wa kienyeji, madai yaliyopingwa na watu mbalimbali, zikiwemo taasisi za kutetea haki za binadamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari,  akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, alidai mzazi  huyo  alitenda uhalifu huo Agosti 20, mwaka huu ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi, Agosti 26.
Ilidaiwa  siku hiyo ya tukio,  mtuhumiwa huyo  baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake, alimzika kwa siri katika  kibanda  chake anachofanyia shughuli za uganga.
Kamanda Kidavashari alisema mtoto Regina alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika  kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari.
“Ndipo  baba mzazi  wa  binti huyo  alipomchukua marehemu na kwenda kumuuguza kwa siri pasipo mama  yake mzazi kufahamu kwani alimdanganya kuwa mtoto wao amepelekwa  kutibiwa na babu yake mkoani Mwanza,” alisema Kidavashari.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakazi  wa kitongoji hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao, walimtilia shaka mtuhumiwa kutokana na tetesi zilizosambaa kwamba, Regina aliuawa na baba yake mzazi na kuzikwa kwa siri.
Mwenyekiti huyo na wakazi wa eneo hilo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa na kuhoji alipo binti yake, aliposhindwa kujibu wakasema wampekue ambapo alipinga vikali  lakini alipopekuliwa  kibandani kwake  walibaini kuwepo kwa tuta dogo lililokuwa  limechimbwa siku za karibuni.
Wakazi hao walifukua tuta hilo  na kukuta kichwa cha mtoto Regina na ndipo wakalitaarifu jeshi la polisi.
Mama wa marehemu, Maria Exavery (22) alisema hakupewa taarifa kwamba binti yake  amekufa.
“Mimi nilikuwa nafahamu Regina yuko kwa babu yake Mwanza akitibiwa,” alisema huku akimwaga machozi.
Naye Regina Kaboni (40), mkazi wa Isamilo Mwanza  ambaye alikuwa akitibiwa na mtuhumiwa,  anadai kuwa alishirikishwa katika maziko ya binti huyo baada ya kufa.“Hata hivyo, nilishtushwa sana kwa kitendo cha mtuhumiwa kumzika  mwanaye  bila mkewe, nilipomuuliza akadai mila za kwao mtoto aliyezaliwa  kwa kutanguliza makalio, mama mzazi  wa mtoto ni mwiko kushirikishwa katika maziko.
Kwa mujibu wa Kidavashari watu wanne, wakiwemo  wazazi  wa marehemu  wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ambapo watafikishwa mahakamani mara tu  baada ya upelelezi kukamilika.
Wengine wanaoshikiliwa na jeshi hilo  ni Regina Kaboni na Msolwa Jacob (29), mkazi wa Kitongoji cha Mwikang’ombe.
CHANZO; GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate