EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, September 15, 2014

CHAZ BABA NUSURA AMUUE MKEWE!

CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba’ anadaiwa nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya kumpiga  na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.
Mke wa ndoa wa 'Chaz Baba', Rehema Sospeter Marwa akiwa na majereha kichani.
MANENO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo karibu na wanafamilia hao (jina limehifadhiwa), usiku wa Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar kilishuhudia ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia nani anamshushia kipondo mwenzake.

Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.

“Dah! Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana,” kilidai chanzo hicho.
MKE AFUNGUKA ‘EI TU ZEDI’
Baada ya taarifa hiyo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta mwanamke huyo ili aeleze nini kilitokea hadi mumewe kutaka kumkatishia maisha.“Nakumbuka siku ya tukio nilikuwa supermarket maeneo ya Mwananyamala A (jijini Dar) nikinunua unga wa ulezi wa mtoto, ghafla Chaz alitokea, akaniamuru niingie kwenye gari alilokuwemo, tukaondoka kuelekea nyumbani.

Rehema Sospeter Marwa akionesha majeraha aliyoyapata mkononi.
“Tulipofika maeneo ya Kinondoni, pale Meridian ndipo niliposhtukia naanza kupigwa. Nakumbuka nilipigwa hadi nikaishiwa nguvu mpaka akatokea rafiki wa Chaz, Hassan Kisanora na kuniokoa, nikakimbilia nyumbani,” alisema mwanamke huyo.
CHAZ ATOWEKA, ARUDI NA SAMAKI MKUBWA
Akiendelea kuzungumza, mke huyo alisema: “Siku hiyo Chaz aliondoka na hakurudi nyumbani mpaka alfajiri. Aliporudi aliniambia amekuja na samaki mkubwa, yuko kwenye friji huku akisahau kuwa amenikosea na anatakiwa kuniomba msamaha.

“Sikumjibu, ndipo alipochukua kitu kizito na kunipiga nacho kichwani, baada ya hapo damu nyingi zikaanza kunitoka hadi puani, niliishiwa nguvu na kupoteza fahamu.”
“Nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali kwa Dk. Mvungi, Kinondoni. Licha ya kwamba nampenda sana lakini alitaka kuniua, hata sijui kisa.”

Majeraha aliyoyapata baada ya kipigo kutoka kwa mume wake.
MADAI YA KUSHANGAZA; NDANI YA MIEZI TISA KICHAPO MARA 16
Katika kuweka mambo zaidi hadharani, mwanamke huyo aliyebahatika kupata mtoto mmoja na mumewe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, tangu afunge ndoa na Chaz miezi tisa iliyopita, ameshachezea kichapo mara kumi na sita hivyo amechoka kufanywa ngoma.“Nimechoka kufanywa ngoma na Chaz, ndoa ina miezi tisa tu nishapigwa mara kumi na sita kati ya hizo nimezimia mara saba kama vipi bora afanye utaratibu anirudishe kwetu,” alimalizia kusema.

CHAZ BABA, IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kupata maelezo ya mke, Ijumaa Wikienda lilimsaka kwa njia ya simu Chaz mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ya mkewe kudai alimpiga ambapo alipopatikana alifunguka hivi:
“Ni wivu tu kaka! Unajua mke wangu ana wivu mkali sana, alianza kunipiga yeye mimi ndiyo nikamrudishia, hakukuwa na sababu nyingine yoyote zaidi ya wivu,” alisema Chaz bila kufafanua.

SERIKALI YALAZIMISHA WATU KUFANYA MAZOEZI.
Serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) imewalazimisha watu kufanya mazoezi ya lazima baada ya kufunga kituo cha daladala cha Mwenge jijini Dar.

'Chaz baba' akiwa na mke kanisani siku ya ndoa yao.
Gazeti hili limekuwa likishuhudia umati wa watu asubuhi kati ya saa 1:00 na 2:00 wakitembea kutoka Makumbusho hadi Mwenge, hali iliyotafsiriwa kuwa serikali imewalazimisha kufanya mazoezi bila hiyari yao.
 Wakizungumzia hilo, baadhi ya raia wanaofanya kazi maeneo ya Mwenge na Mikocheni eneo la viwanda, wamesema baada ya kufungwa kwa kituo hicho, wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu asubuhi hivyo kuwafanya wanapofika maeneo yao ya kazi wawe wametoka jasho sana.

“Unajua asilimia kubwa ya tuliokuwa tunashuka Mwenge ni wa kipato cha chini, sasa baada ya kuhamishiwa Makumbusho, tunalazimika kutembea hadi Mwenge. “Tunachukulia kama ni mazoezi kwani baadhi tangu kuhamishwa kwa kituo hicho sasa hivi vitambi vimepungua kwa kutembea bila kupenda,” alisema Salum Juma wa Mbagala.
Naye John Katuvi alisema: “Huku ni kulazimishwa kufanya mazoezi, mimi nadhani serikali ifikirie upya uamuzi wa kuondoa kituo kile pale.“Ujue siyo wote tunaweza kushuka Makumbusho na kuchukua tena usafiri mwingine, ndiyo maana asubuhi utaona umati wa watu ukitembea, ukiwaona utadhani wanafanya mazoezi kwa kupenda kumbe hawana nauli ya kuunganisha magari.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate