EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, September 15, 2014

JAJA KIDUME


Geilson Santana ‘Jaja’ akishangilia goli na wachezaji wenzake.
Hans Mloli na Sweetbert Lukonge
TAMKA jina Jaja upate fedha! Tamka jina la Jaja uwape Yanga furaha! Tamka jina Jaja upate shangwe Jangwani! Mara baada ya mechi dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, jana jijini Dar es Salaam, Wanayanga wote walikuwa wakitamka jina la straika huyo Mbrazili aliyekuwa msaada mkubwa kwa timu yao kupata ushindi wa mabao 3-0.


Yanga imetwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam idadi hiyo ya mabao huku Geilson Santana ‘Jaja’ akifunga mabao mawili, moja likiwa la ufundi kiasi kwamba kuna mashabiki wa timu pinzani walisimama na kumpigia makofi.
Kwa ushindi huo wa kuukaribisha msimu mpya wa 2014/15, Yanga imeamsha morali ya mashabiki wake ikiwa ni siku chache baada ya kupata pigo la kumpoteza Emmanuel Okwi ambaye ametua Simba.
Yanga ikiongozwa na Kocha Marcio Maximo raia wa Brazil katika mchezo huo uliojaza watu kibao, ilionyesha soka zuri licha ya kubanwa katika kipindi cha kwanza na Azam ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.
Azam ilianza mchezo huo kwa kasi huku kukiwa na mashambulizi ya kupokezana pamoja na kosakosa za hapa na pale, lakini mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika, hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Mrisho Ngassa wa Yanga ambaye alibadilishana jezi na nahodha wa Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wakati wa kuelekea mapumziko, alikuwa na makeke kadhaa kwenye kipindi hicho lakini alikuwa akikutana na kigingi cha beki mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, David Mwantika.
Mpaka wanaenda mapumziko, Jaja alikuwa amepiga pasi 8, mipira ya vichwa 5, akiotea mara 2, ambapo pasi moja iliharibika, tofauti na straika wa Azam, Didier Kavumbagu ambaye alipiga pasi 11, vichwa 2, mashuti 2 golini lakini hakuotea.
Yanga walianza kufurahi katika dakika ya 56 baada ya Jaja kuunganisha pasi nzuri ya Simon Msuva huku mabeki wa Azam wakibaki wanatazamana.
Furaha ikiwa haijapoa, Jaja aliipatia Yanga bao la pili baada ya kufunga kiufundi katika dakika ya 65. Alipata mpira ndani ya 18, akafanya kama anapiga shuti, kipa wa Azam, Mwadini Ally, akajiandaa, lakini Mbrazili huyo akapiga kwa ‘kuuchop’ kidogo, hivyo Mwadini kujikuta akiutazama ukimpita kwa juu na kuingia wavuni taratibu.
Baada ya hapo, Yanga iliendelea kucheza soka zuri lakini alikuwa ni Jaja ambaye alipata shangwe nyingi hasa baada ya kupiga pasi za visigino, vitendo vilivyokuwa vikisababisha mashabiki kulipuka kwa furaha.
Simon Msuva alihitimisha furaha ya Yanga baada ya kufunga bao lililotokana na makosa ya Mwadini ambaye alienda kuupiga mpira akaukosa, kitendo kilichomfanya Msuva kubaki na lango, akautupia mpira kama hataki.
Katika mchezo huo kulikuwa na mabadiliko kadhaa kwa timu zote ambapo Yanga iliwatoa Said Juma na kuingia Hassan Dilunga, Nizar Khalfan akaingia Msuva, Jaja akapumzika na kumpisha Hussein Javu, Haruna Niyonzima alimpisha Hamis Kiiza.
Azam alitoka Leonel akaingia Hamis Mcha, Himid Mao alitoka na kuingia Kelvin Friday, Erasto Nyoni alipumzika na kuingia Gadiel Michael, Kipre Tchetche alimpisha Ismail Diarra. 
Moja ya matukio yaliyowashangaza wengi ni kitendo cha Leonel raia wa Haiti alipotolewa kupitiliza moja kwa moja vyumbani badala ya kukaa kwenye benchi kama wenzake.
Baada ya mchezo kocha Marcio Maximo alisema: “Nafurahia ushindi na nawashukuru mashabiki waliojitokeza, Azam wana kikosi kizuri lakini nafurahi tumepata ushindi.”
Kwa upande wake Jaja alisema, “Nimefurahi baada ya kufunga mabao haya, nitajitahidi kuhakikisha kila mechi nafunga mabao.”
AZAM: Mwandini Ali, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, David Mwantika, Aggrey Morris, Michael Balou, Himid Mao, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbagu, Kipre Tchetche na Leonel Saint-Preux.
YANGA: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Said Juma, Haruna Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Nizar Khalfan.
CHANZO: CHAMPIONI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate