Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO
mpya wa Yanga SC, Mbrazil Andrey Coutinho aling’ara katika mechi za
kirafiki za timu hiyo visiwani Zanzibar akifunga mabao mawili katika
michezo mitatu.
Na alifunga mabao mazuri Uwanja wa Amaan, Zanzibar moja kila mchezo, Yanga SC ikishinda 2-0 mara zote dhidi ya Shangani na KMKM.
Zaidi
ya kufunga mabao, Coutinho alionyesha uwezo mkubwa mno wa kucheza soka-
kwa ujumla umiliki wa mpira, kasi, utoaji wa pasi, upigaji krosi, kona
na mashuti ya mbali.
Alionyesha
uwezo wa kupasua katikati ya wachezaji wa timu pinzani na kufumua
mashuti ya kushitukiza na kufunga mabao yake hayo mawili mazuri.
Kwa
mashabiki wa Yanga SC wa Dar es Salaam waliosikia sifa za Coutinho
Zanzibar, bila shaka leo itakuwa fursa nzuri kwao kujionea wenyewe juu
ya Mbrazil huyo.
Watapata
fursa hiyo wakati Yanga SC ikimenyana na Thika United ya Kenya katika
mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezaji
mwingine mpya wa Yanga SC kutoka Brazil, Geilson Santana ‘Jaja’ ambaye
pamoja na kufunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Chipukizi
Uwanja wa Gombani, Pemba hakuvutia sana kiuchezaji, naye atakuwa na
nafasi nyingine ya kudhihirisha uwezo wake kwa wana Yanga wa Dar es
Salaam.
Kwa
ujumla kocha mpya, Mbrazil, Marcio Maximo atahitaji kuendeleza rekodi
ya ushindi baada ya kushinda mechi zote tatu za kujipima nguvu Zanzibar.
Kifaa cha ukweli; Andrey Coutinho aling'ara na Yanga SC Zanzibar, je leo ataendelea cheche zake Taifa? |
No comments:
Post a Comment