Msanii wa Bongo Muvi, Mariam Juma ‘MC Chimamy’ enzi za uhai wake.
Mauti hayo yalimkuta MC Chimamy wikiendi iliyopita baada ya
kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, akiwa tayari na
hali mbaya kwani kabla ya hapo alianzia Hospitali ya Palestina, Sinza
ambapo alilazimika kukimbizwa katika hospitali hiyo ya Wilaya ya
Kinondoni ili kunusuru maisha yake na kiumbe alichokuwa nacho tumboni.Msiba huo umezua simanzi kubwa kwa wasanii wenzake hasa Vanita Omary, Halima Yahya ‘Davina’, Yvonne-Chery Ngatwika ‘Monalisa’, Mariam Kakwaya na wengine kwani alikuwa ni mtu wao wa karibu na siku aliyokutwa na umauti alikuwa amepangwa kuwa mshereheshaji wa shughuli ya Davina ya kibao kata iliyofanyika Bamaga-Mwenge, Dar.
“Msiba huu umenishtua sana, sikutarajia kama Chimamy angetutoka kimchezo hivi, ukweli nimeumia sana na sina la kusema, namshukuru Mungu kwa kazi yake,” alisema Vanitha.
No comments:
Post a Comment