EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, September 20, 2014

MTOTO WA MCHUNGAJI, MWANAKWAYA KANISANI WANASWA KICHAKANI

Na Francis Godwin, Iringa “UTAN’TAMBUAJE
kama nimeokooka, utantambuaje kama namuheshimu Mungu…”
Wimbo huu wa Injili ulioimbwa na Bony Mwaitege wengi hupenda kuusikiliza kama burudani lakini una ujumbe mzito hasa kwa wale wanaosema wameokoka.
Wanakwaya wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, Hanipher na Godfrey (mtoto wa mchungaji) walionaswa wakiwa kichakani.
Hivi karibuni mjini Iringa, wanakwaya wawili wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God, mwanamke alijitambulisha kwa jina moja la Hanipher na mwanaume aliyesema anaitwa Godfrey, walinaswa usiku kichakani katika mazingira yaliyojaa utata, Risasi Jumamosi linakupa kisa kamili.

NI MAKABURINI
Tukio hilo la kushangaza, lilijiri kwenye eneo la Makanyagio ambalo lina makaburi ya awali katika Manispaa ya Iringa licha ya kuwepo na nyumba za wenyeji pia.
KAZI YA SUNGUSUNGU
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanakwaya hao walinaswa na sungusungu ambao siku za hivi karibuni wamekuwa wakifanya ‘patroo’ katika eneo hilo na la Isoka kufuatia kuwepo kwa matukio ya wakazi wake kuvamiwa, kupigwa na kuporwa mali.
SIKU YA TUKIO
Siku ya tukio, sungusungu  hao wakiwa katika majukumu yao  waliwaona  wanakwaya hao wakiacha njia kuu na kuchepukia porini umbali unaokadiriwa kuwa mita 20 kutoka barabarani.
“Ilibidi sungusungu wawafuate hadi kule kichakani, ndipo walipowakuta katika mazingira tata na yenye maswali mengi bila majibu. Mbaya zaidi, yule mwanamke alikuwa na mtoto wa mwaka mmoja mgongoni,” kilisema chanzo chetu.
Wanakwaya wakifunguka kueleza kisa cha kuwa kichakani usiku mnene.
WAPEWA KICHAPO, WAJIANIKA
Chanzo kikadai kuwa, sungusungu hao waliwapa kichapo chepesi ili waweze kusema walikuwa wakifanya nini na wao ni akina nani, ndipo mwanamke huyo akaweka wazi mambo kwamba, yeye ni mkazi wa Kitongoji cha Isoka ilhali kijana huyo ni mwimbaji mwenzake wa kwaya lakini pia ni mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo.
ETI?
Katika hali ya kushangaza, mtoto huyo wa mchungaji huku akiomba samahani kwa kunaswa kichakani, alisema eti kilichowapeleka huko muda huo wa usiku ni kumsaidia mwanamke huyo kumwingizia nyimbo za dini kwenye simu yake!!
AKIRI SI MWENENDO MWEMA
Pamoja na yote, Godfrey  alikiri kuwa kitendo cha kuingia kichakani na mwanamke muda huo wa saa 2.15  usiku kilikuwa ni hatari kwao kiimani na hata usalama wa miili yao kwa ujumla.
Kiimani alikuwa na maana kwamba, kuonekana kichakani watu waliookoka hakutoi picha nzuri kwa jamii inayotakiwa kuhubiriwa ili watu wamrudie Mungu, usalama wa miili ni kama vile kuumwa na nyoka au wadudu wengine wenye kudhuru.
SUNGUSUNGU NAYE
Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa sungusungu hao alisema haikuwa rahisi kwao kuamini kwamba wawili hao waliingia kichakani kuingiziana nyimbo kwenye simu.
“Hivi kweli mtoke barabarani muingie kichakani kisa kuwekeana nyimbo kwenye simu, inaingia akilini kweli? Labda bwana,” alisema sungusungu huyo bila kutaja jina lake akidai wana bosi wao ndiye alitakiwa kusema. Baada ya kuwatembezea kichapo na wawili hao kuomba msamaha, sungusunga hao waliachia na kuwaonya wasirudie tena kukutwa vichakani usiku.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate