REKODI zilizopatikana kutokana na usajili wa
ligi mbalimbali za Ulaya umekuwa ukipishana lakini kwa idadi ndogo sana na hii
inatokana na vyombo vya habari au wale wanaozitoa kwao wanavyowahabarisha.
Kikubwa cha kujadili ni namna ambavyo England
imeingia kwenye njia nyingine kabisa kutokana na timu zake kutumia idadi kubwa
ya fedha katika usajili hadi kufikia kuzitupa mbali ligi za Hispania ‘La Liga’
na Italia ‘Serie A’ ambazo zimekuwa ziking’ara kutokana na kutumia fedha nyingi
katika usajili.
Katika
kipindi cha misimu miwili, klabu za England, Tottenham Hotspur na Liverpool
ziliwauza Gareth Bale na Luiz Suarez kwa vigogo wa Hispania, Real Madrid na
Barcelona.
Hadi sasa biashara ya Bale ndiyo uhamisho
ghali zaidi kwa kuwa aliuzwa kwa pauni milioni 85, Suarez naye ni kati ya
uhamisho ghali kwa kuwa ni pauni milioni 75.
Msimu uliopita wa 2013-14, klabu za England
zilitumia pauni milioni 760, lakini msimu huu gharama zimepanda maradufu hadi
kufikia pauni milioni 857 ambayo imevunja rekodi ya misimu yote tangu
kuanzishwa kwa ligi hiyo.
Misimu miwili sasa, Premier League
imebadilika, badala ya kuuza wachezaji tu Hispania imekuwa ikinunua tena kutoka
La Liga na kwa bei ghali.
Arsenal imefanya hivyo misimu miwili mfululizo
ikianza kumnunua Mesut Ozil kutoka Real Madrid na msimu huu ikamnunua Alexis
Sanchez kutoka Barcelona wakati Man United ilimtwaa Ander Herrera kutoka
Athletic Bilbao, kisha ikamnasa Angel Di Maria kutoka Real.
Lakini hiyo haitoshi, Premier League sasa
ndiyo ligi ghali zaidi kutokana na kutumia fedha nyingi za usajili mara mbili
ya La Liga ambayo inashika nafasi ya pili.
Usajili wa La Liga ambayo inawajumuisha vigogo
Real Madrid na Barcelona, umegharimu zaidi ya pauni milioni 434 wakati Serie A
ina pauni milioni 272 zilizotumika kwa ajili ya manunuzi ya uhamisho wa
wachezaji.
Bundesliga yenyewe imetumia pauni milioni 261 wakati Ufaransa
kupitia klabu zao mbili kubwa, angalau walijisukuma na kufikia hadi pauni milioni
112.
Hii utaona kiasi gani Premier League imegeuka
kuwa ligi maarufu lakini pia inayotumia fedha nyingi na zaidi klabu tano za juu
ndizo zimetumia fedha nyingi.
Manchester United ndiyo imeongoza kwa kumwaga pauni
milioni 153.1, Liverpool inafuatia kwa kutumia pauni milioni 116.8, Chelsea
(pauni milioni 87.7), Arsenal (pauni milioni 78.2), Southampton (pauni milioni
57.9) na Man City (pauni milioni 54.5).
No comments:
Post a Comment