Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba akifungua
Semina ya Kamata Fursa Jitathimini, Jiamini kisha Jiongeze mapema leo
kwenye Ukumbi wa Bwaro la Magereza mjini Musoma.
Baadhi ya wakazi wa Musoma wakifuatilia kwa makini semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Bwalo la Magereza.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya akiteta jambo na Ruge wakati semina ya Kamata Fursa ikiendelea.
Msanii
Lameck Ditto akiwapa mbinu mbalimbali wakazi wa Musoma ili wapate
kujikwamua kiuchumi kama alivyoweza yeye kupigania maisha yake.
MPANGO wa Serengeti Fiesta Kamata Fursa leo
umefanyika kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa mji wa Musoma ambapo baadhi
ya watu mashuhuri walipata nafasi ya kuongea na wakazi hao na kuwapatia
mbinu mbalimbali watakazoweza kufanya kwa ajili ya kujikwamua katika
shughuli zao za kiuchumi.Akizindua Semina ya Kamata Fursa Twenzetu, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba alisema kuwa, leo ilikuwa ni siku mwafaka kwa kuwaonyesha fursa mbalimbali zilizopo mjini Musoma.
Kwenye Semina hiyo pia Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya alipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa Musoma na kuwapatia mbinu mbalimbali zitakazowawezesha kujikwamua kimaisha kupitia njia ya biashara ya kilimo cha kila mwaka.
Pia msanii wa Bongo Fleva, Lameck Ditto naye alipata muda mwafaka wa kuzungumza kwa kifupi na wakazi wa mkoa huo na kuwataka waongeze bidii kwenye shughuli zao za kila siku kwa kuwa anaamini mafanikio ya mtu yanatokana na juhudi binafsi, ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali mbalimbali zilizopo sehemu husika.
(HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/ GPL, MUSOMA)
No comments:
Post a Comment