EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, September 4, 2014

YANAYOWEZA KUMFANYA MPENZI WAKO AKATEMBEA NA RAFIKI YAKO!


Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana tena kupitia safu hii nikiamini umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.
Mimi namshukuru Muumba wa mbingu na ardhi kwa kuniwezesha kutimiza majukumu yangu ya kila siku likiwemo hili la kuelimishana na kukumbushana juu ya mambo yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi.
Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita nilikuwa na kazi kubwa ya kumshauri rafiki yangu ambaye aliniletea mashitaka ya mpenzi wake kutembea na rafiki yake.

Nilipata wakati mgumu sana kwani nilipoongea na msichana akaniambia wazi kwamba, amekuwa hapati penzi alilotarajia kutoka kwa rafiki yangu.

Msichana huyo akaenda mbele zaidi na kusema kwamba, yule shemeji yake alionesha kumjali sana kiasi kwamba siku alipomtamkia kwamba anampenda ilimuwia ngumu kukataa.
Kuna kitu cha kujifunza hapa kwamba endapo utaishi na mpenzi wako bila kumdhihirishia kwamba unampenda kwa dhati, akitokea mtu wa pembeni akaonyesha kuwa kafa kaoza, tarajia kusalitiwa kama siyo kuachwa kwenye mataa.
Unapokuwa umeanzisha uhusiano na mtu, utambue ana watu wengi wanaomtaka lakini huenda anawakatalia kwa kuwa yuko na wewe, sasa ukionesha kutomjali, hawezi kuendelea kuwa muaminifu kwako. Atachepuka na hata kama ataendelea kuwa na wewe ni kwa kuwa labda hana ujasiri wa kukuacha.
Ndiyo maana leo nikaona nikupe sababu ambazo zinaweza kumfanya mpenzi wako akatembea na rafiki yako tena wakati mwingine kwa siri bila wewe kujua.
Wewe mwenyewe
Endapo utakuwa umeanzisha uhusiano na mtu, wewe mwenyewe unaweza kutengeneza mazingira ya kusalitiwa. Usipoonesha kumpenda, kumjali, kuthamini penzi lake kisha rafiki yako akayaonesha hayo kwake, ni rahisi sana kukupiku.

Kwa mfano, endapo umekuwa na mpenzi wako lakini hata siku moja hujawahi kumpa zawadi au kumtoa ‘out’, siku shemeji yake (rafiki yako) akiamua kufanya hivyo, mpenzi wako atahisi yeye ni mtu sahihi kwake.
Kujirahisi kwake
Wapo ambao wanatembea na mashemeji zao kwa sababu tu ya kujirahisi kwao. Kwa mfano unapopendelea kuzungumza mambo ya chumbani na rafiki wa mpenzi wako unatarajia nini? Unapomvalia kihasara rafiki wa mpenzi wako lengo linakuwa ni lipi?
Mbaya zaidi ni pale utakapokuwa na mashemeji ambao hawabipiwi. Hapa namaanisha wale ambao wakiona dalili ya kupendwa tu, wanaomba chansi.

Kumuamini sana
Haishauriwi kumuamini sana rafiki yako kwani wengine wakipewa uhuru wa kuwa karibu na mashemeji zao, huchukulia kama fursa ya pekee.
Kwa mfano, unapomuamini rafiki yako kiasi cha kumruhusu aende na mpenzi wako baa, klabu au ufukweni ni kujitafutia matatizo.

Tunajua kwamba wapo marafiki waaminifu lakini tambua tu kwamba wengi wanapokuwa katika mazingira hayo ndipo huishia kusaliti na wakati mwingine bila kupenda.
 Kwa nini nasema bila kupenda? Chukulia umemruhusu mpenzi wako aende baa na rafiki yako, wamekunywa pombe hadi wamelewa kisha rafiki yako anamchukuwa mpenzi wako kwenye gari kumrudisha nyumbani.

Wengi kwenye mazingira hayo uzalendo unawashinda. Kwa hiyo kama hutaki yakukute ya kusalitiwa, kama una tabia ya kumruhusu mpenzi wako kwenda baa na shemeji yake, acha mara moja.
Rafiki mnafiki
Unaweza kuwa na rafiki lakini kumbe ni mnafiki. Huyu ni yule ambaye mko pamoja lakini anajiapiza kwamba siku moja lazima atakuchukulia mpenzi wako. Huyu ndiye tunamuita rafiki mnafiki.

Kutokana na tabia hizo ndiyo maana matukio ya baadhi ya wanaume kuwatongoza wapenzi wa marafiki zao yamekuwa yakiongezeka. Pia wanawake wengi sasa hivi hawaoni hatari kuwatongoza marafiki wa wapenzi wao au wapenzi wa mashoga zao.
Penzi la kweli
Mfano Juma ana mpenzi wake aitwaye Asha na Juma ana rafiki yake aitwaye Jamali. Juma na Asha ni wapenzi lakini hawapendani kivile ila Jamali anaonekana kuwa na penzi la kweli na Asha na wakati huohuo Asha naye anahisi kuwa na penzi la kweli na Jamali.

Katika mazingira hayo usije ukashangaa siku moja kusikia Asha katembea na Jamali. Siyo kutokana na tamaa au ushawishi bali ni kutokana na uwepo wa penzi la dhati kati yao.
Katika mazingira haya ndipo ambapo tumekuwa tukisikia fulani kamuacha mkewe kisha yule mke kaolewa na mwanaume ambaye alikuwa rafiki wa wanandoa hao.

Tamaa tu
Endapo utagundua mpenzi wako katembea na rafiki yako, kuna uwezekano ameshawishiwa kwa pesa au mali. Hii ni kwa sababu wapo watu ni dhaifu sana, yaani wao kusaliti wapenzi wao kwa sababu ya pesa, mali au tamaa zao za kimwili siyo kitu kigumu.

Ndiyo maana tunashauriwa kuwa na wapenzi ambao hawana tamaa za kijinga. Katika siku za mwanzo za uhusiano wenu ukigundua uliyenaye si mtu wa kuridhika na penzi unalompa, pesa na mali mlizonazo, mapema muonyeshe mlango wa kutokea kwani itakuwa siyo jambo la ajabu kusikia katembea hata na ndugu au rafiki yako.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate