Picha
ya juu na chini wananchi wa jiji la Arusha waliojitokeza kuuangalia
mwili wa jambazi huyo atari aliowawa na polisi usiku wa kuamkia leo.
Wananchi wakiendelea kushuhudia mwili wa jambazi hilo nje ya jengo la makao makuu ya polisi mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la Glock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia.
Jambazi
mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abudallah alimaarufu kwa jina
la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa Moivo ameuwawa baada ya kupigwa
risasi katika majibizano na askari wa jeshi la polisi.
Akizungumzia
tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa
tukio hilo limetokea October 10 mwaka huu majira ya saa nane na dakika
nne usiku katika kijiji cha Moivo kilichopo ndani ya kitongoji
cha Enaboishu wilayani Arumeru.
Alisema
kuwa marehemu Ramadhan Abdallh aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na
jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo
yameshawahi kutokea ndani ya mkoa huu pamoja na katika maeneo
mbalimbali ya nchi hiii.
Alibainisha kuwa
kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na juhudi na kutumia mbinu za
kisasa za kiyupelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu)
ambapo askari polisi walimwamuru ajisalimishe lakini alikaidi amri na
kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu
mashambulizi na kumsababishia umauti kumfika.
“Mara
baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa mwili wa
marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba
RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14)
ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano
yarisasi na mbali na hapo polisi pia walifanya upekuzi katika chumba
cha jambazi hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na
magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja
,Radio call moja yeye nembo ya ITSS/UNICTR pamoja na pikipiki aina ya
toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU pamoja
na kofia ngumu”alisema Sabas
Aidha
alibainisha kuwa pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi
hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki
yenye namba za usajili T 805 CVD ambapo alibainisha kuwa jambazi hili
lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara pamoja
na chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla
yakupiga risasi (Glock Fab Defence moja),kifaa cha kusafishia bastola
pamoja na koti kubwa jeusi.
Kamanda
Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili
lilishayafanya kuwa ni pamoja na tukio lililotekea Augast 6 majira ya
saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa akiwa na
mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke
aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina
wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake ,hu ku tukio lingine likiwa
limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo yaoasiti ambapo jambazi huyo akiwa
na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi yam domo na
kutokea kichwani mototo aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka
mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi
kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
Kamanda
sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi
nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na
kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.
“arusha
sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali
kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na
napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga
vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia
waendelee kuwafichua wahalifu popote pale ili tuwaangamize
kabisa”alisema Sabas
Mmoja
wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo
Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili
alilipongeza jeshi la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo
kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi
walivyokuwa wanauwa watu.
habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
No comments:
Post a Comment