Stori: Hamida Hassanna Gladness Mallya
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima, inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu ‘Mkongo’ ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ‘kumalizana’ na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.

Akizoza na gazeti hili ndani ya Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki,
Dar, mapema wiki hii, Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka
kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni
mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi
kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si
vinginevyo.
“Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper, Husna mara Wema, si
kweli, hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi (Kenya) kwa lengo la
kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata
nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu,” alisema Mwami bila soni.
Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea
huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa
kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa
ndoto zake.
“Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena
sana,” alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha
zimemtembelea.
Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo
hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na
hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar, hakuwepo hivyo juhudi
za kumpata zinaendelea.
No comments:
Post a Comment