EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, October 17, 2014

POLISI, WAANDISHI NANI WAZUSHI UTEKAJI WATOTO DAR?

WIKI iliyopita vyombo vya habari likiwemo gazeti la hili viliandika habari ya Jiji la Dar es Salaam kutikiswa na wimbi la utekaji watoto ambao wamekuwa wakichukuliwa katika mazingira ya kutatanisha huku wengine wakiuawa na kunyofolewa sehemu zao nyeti.
Msingi wa habari hiyo ulikuwa ni kutoa tahadhari kwa wazazi na vyombo vya dola kuchukua hatua ya kujilinda na uhalifu huo mpya.
Lakini pamoja na wema wa habari hizo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kupitia kwa kamanda wake Camilius Wambura, waliziita habari hizo kuwa ni za kizushi huku wakionya kuwachukulia hatua wanaoeneza uzushi huo.
Tafakuri ya kawaida kuhusu onyo la uzushi huo iliwahusu waandishi wa habari wakiwemo wa gazeti la hili. Kusudio la polisi kwenye tamko hilo linaweza kuwa na tafsiri nyingi lakini moja kati ya hizo ni kuwaambia wananchi wawapuuze waandishi.
Wakati sura ya jeshi la polisi hasa Kinondoni ikiwa na picha hiyo ya uzushi wa waandishi, tukio la mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Msingwa iliyopo Kimara-Temboni, wilayani Kinondoni jijini Dar eneo la kazi la Kamanda Wambura, alitekwa mwishoni mwa wiki iliyopita, akauawa kisha kunyofolewa sehemu zake za siri.
Katika mazingira hayo swali la mzushi ni nani kati ya waandishi wa habari na polisi limepata jibu. Hata hivyo, haliwezi kuwa jambo la kufurahia kupata ushindi wa uzushi bila kujiuliza kasumba ya polisi kuwaita waandishi wazushi kaianzisha nani na kwa manufaa gani.

Vita ya kugombea fito kwenye ujenzi wa nyumba moja kaibuni nani? Maana ushirikiano kati ya jeshi la polisi na waandishi unazidi kuzorota kila siku, hakuna anayeona hatari inayolikabili taifa siku za usoni kama hali hii itaendelea kuota mizizi.
Ni juzi tu waandishi wa habari wamepigwa na polisi wakati wakitekeleza majukumu yao, mzozo umepoa kimtindo lakini moshi ungali ukifuka.Hata kama jeshi la polisi halitaki kushaurika kwa dalili zinavyojionesha hivi sasa kwa waandishi kuhojiwa, kutishwa na kusukwasukwa kwa baadhi ya habari kutafsiriwa vibaya na jeshi hili;  bado wanahabari wana jukumu la kuitumia jamii bila hofu.
Ushauri wangu kwa jeshi la polisi lenye sura hii ni kwamba, haliwezi kupata mafanikio ya kweli ya kuwalinda raia na mali zao bila kuwa na ushirikiano wa kutosha na vyombo vya habari. Hilo naweza kuliapia!
 Taarifa za matukio zimekuwa zikiripotiwa kwa wingi zaidi kwenye vyombo vya habari kuliko polisi ambako kumejaa lawama za “ukipiga simu hawapokei” na woga wa watoa habari kugeukwa pindi wafikishapo ripoti zao polisi.  Anayebisha katika hili shauri yake.

Wahariri ni mashahidi wa hiki nisemacho, wao wamekuwa watu wa kwanza kupewa taarifa za ajali licha ya kuwa siyo trafiki, huambiwa habari za wauza madawa ya kulevya ingawa wao siyo polisi, watu kujihusisha na ujambazi hata kama wao siyo askari kanzu! Yote hii ni ushahidi wa kuaminika kwao.
Sasa ukiona jeshi la polisi halitaki ushirika na waandishi wenye wingi wa taarifa za matukio kama nilivyosema ni dhahiri kwamba hawataki pia kupata ripoti zitakazowasaidia kufanikisha ulinzi wao kwa jamii.
Mwenye hasara ni nani,  ni waandishi au polisi wenye jukumu la ulinzi? Vyombo vya habari viliandika utekaji watoto vikamaliza kazi yake, Wambura alipokuja na kauli ya uzushi leo yeye ndiye anayenyooshewa vidole, siyo waandishi. Ningekuwa kijana ningesema Wambura anatakiwa kujiongeza.
Nachochea tu!

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate