EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, October 7, 2014

WASAKATONGE COMEDY SHOW NDANI YA AZAM TV YASAKA WAKALI WA UCHEKESHAJI, USAHILI KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA DAR!


DUNIANI kote! watu hujipatia fedha nyingi na kujenga heshima kubwa ndani na nje ya nchi zao kupitia vipaji walivyojaaliwa na Mungu muumba.
Watu kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Wayne Rooney, Yaya Toure, Didier Drogba na wengineo, wana utajiri mkubwa kupitia miguu yao iliyobarikiwa kutandaza soka.
Hata Tanzania kuna wanasoka wengi wanaovuna mamilioni ya fedha kupitia vipaji vyao.
Mbali na soka, wengine wana vipaji vikubwa vya muziki , uchekeshaji, maigizo na taaluma mbalimbali.
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaa vijana wengi wenye vipaji vikubwa katika mambo tofauti tofauti, lakini fursa ya kuonekana imekuwa adimu sana.
Ni kawaida kabisa kupita mitaani na kuwakuta vijana wenye uwezo wa kuchekesha na kuigiza, lakini hawana kwa kwenda.
Kwa kulitambua hilo kituo bora cha Azam TV kimedhamiria kutoa fursa kwa watu wote wanaojihisi wana vipaji vya uchekeshaji, lakini hawajapata nafasi ya kuonekana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Katika kuhakikisa hilo, Azam TV imeandaa kipindi cha ucheshi cha Luninga kiitwacho WASAKATONGE COMEDY SHOW na usahili kwa ajili ya kutafuta wenye vipaji vya kuchekesha jukwaani na kuigiza vichekesho unatarajia kufanyika ijumaa ya Oktoba 10, 2014, kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni ndani ya uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Usahili huo utajali misingi ya haki na mwenye uwezo pekee ndiye atakayepata nafasi ya kusonga mbele, hivyo kila mtu afike kujaribu bahati yake.
Mchakato huu utaegemea zaidi katika kigezo cha Ubunifu kwa minajili ya kuchekesha, kuwa mwepesi katika ucheshi, kuwa na mawazo ya haraka katika ucheshi na jinsi gani anaweza kushirikiana na wenzako kama timu moja.
Kwa mshiriki yeyote yule kutoka nje ya mkoa wa Dar es salaam bado ana nafasi ya kushiriki usahili isipokuwa gharama zote zitakuwa juu yake.
Ili kutengeneza timu ya WASAKATONGE mchakato utakuwa wa awamu mbili;-
Mosi; kutakuwa na usahili wa wazi utakaofanyika uwanja wa ndani wa taifa (Indoor); kwa wale wachache watakaopita kulingana na hitaji la kamati watapewa utaratibu juu ya kipi kitakachoendelea kwa mzunguko wa pili.
Pili; kutakuwa na mchujo utakaopelekea kuchaguliwa kwa watu wachache, wasiozidi kumi na hao ndio watakaotengenezwa kwa kupatiwa mafunzo ili kuwa wachekeshaji/waigizaji. Watakaobahatika watakuwa WASAKATONGE wa Azam tv.
Mambo ya Zingatia!!!
Usaili huu ni wa wazi, Wasahiliwa watapaswa kujigharamia usafiri na chakula, Hakuna zawadi kwa washindi. Mafunzo ya uchekeshaji yatatolewa kwa washindi 10
WASAKATONGE, Ni zaidi ya COMEDY

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate