EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, November 6, 2014

KISA FREEMASON MZEE WA UPAKO AMIMINA RISASI MTAANI


CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
NI kama kimenuka tu!
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar,  Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita  alizua la kuzua kufuatia kumimina risasi kadhaa hadharani kwa madai ya kuwatawanya kundi la vijana waliodaiwa kumvamia na kuziba barabara kwa lengo la kumfanyia kitu mbaya.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar,  Anthony Lusekelo  ‘Mzee wa Upako’ akitafakari jambo.
Ishu hiyo iliyojaa utata mkubwa, ilitokea saa nne usiku maeneo ya Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam kwenye barabara inayotoka barabara kuu kwenda kanisani kwake.

MAELEZO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, tukio lilianza kwa Mzee wa Upako aliyekuwa akipita kwa miguu kukejeliwa na vijana waliomwita Freemason kauli ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliiona ni ya kejeli kwake.“Baada ya kuitwa Freemason, yule kijana akiwa na wenzake waliendelea kumkejeli Mzee wa Upako, akawafuata na kuwauliza mbona mnanitukana, nimewakosea nini?”

RISASI ZARINDIMA
“Alipoona wale vijana wanazidi kumkejeli huku wakionesha dalili za kumfanyia fujo ndipo alipotoa bastola yake na kufyatua risasi tatu juu hali iliyowafanya wale vijana kutawanyika huku na kule.

“Baadhi ya watu walikuwa kwenye biashara zao, nao walitimua mbio, wengine waliacha biashara, unajua risasi ni risasi tu, mtu akisikia risasi hawezi kukaa salama hata kama ni mjeshi,” kilisema chanzo hicho.
Moja wapo ya alama zinazoaminiwa kuwa ni za Freemasons
MZEE WA UPAKO ATIMUA MBIO
Ilizidi kudaiwa kwamba, kufuatia kimbiakimbia hiyo, Mzee wa Upako naye alikimbia. Baadaye alirudi eneo la tukio kimachale na kukuta watu wameanza kukusanyika kujua kulikoni.“Mzee wa Upako alipofika aliagiza mtu atakayeokota ‘magazini’ ya risasi alizofyatua angempa shilingi alfu ishirini, vijana wengine wakaingia kazini, wakapata moja, wakapewa chao, Mzee wa Upako akasema mtu akiokota nyingine aipeleke polisi,” kilisema chanzo.

MADAI YA WATU
Kuna madai kwamba, vurugu hizo zilipambwa na kijana mmoja anayeitwa Robert ambapo mtumishi huyo wa Mungu alimkomalia kuwa ndiye aliyekuwa akiongoza wenzake kumtukana na kumkashifu kwamba yeye ni Freemason na si mchungaji wa kiroho kama anavyojiita.

MZEE WA UPAKO NA GAZETI LA AMANI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilimtafuta Mzee wa Upako kwa njia ya simu na alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kueleza ‘full’ mkanda.“Ni kweli lilitokea. Ni kwamba, siku hiyo nilipofika eneo lile kuna vijana wa kihuni walinifuata kwa nyuma, wakaanza kupigapiga gari langu, wengine wakizuia njia huku wakidai eti mimi ni Freemason.

Mfano wa silaha ya moto (bastola) kama  ile ya Mzee wa Upako.
“Nilijaribu kuwaambia kwamba mimi ni kiongozi wa kiroho lakini badala yake wakaanza kuniangushia matusi. Ili kujiokoa nilifyatua risasi hewani kuwatawanya,” alisema Mzee wa Upako.
Alipoulizwa kama anaweza kujua sababu za watu hao kumvamia na kumwambia yeye ni Freemason, kiongozi huyo alisema:

“Siwezi kujua, lakini mara baada ya kufyatua risasi na wao kutawanyika mimi niliamua mwenyewe kwenda Kituo cha Polisi Urafiki (Dar) kutoa taarifa.“Mimi siwezi kujua sababu za watu hao kunikashifu na kunitukana labda ukiwapata watakuambia lakini ni watu ambao naamini wametumwa na mtu f’lani ambaye mimi siwezi kukwambia lakini polisi watamjua baada ya upelelezi wao,” alisema.
Alipoulizwa alikuwa anatoka wapi usiku huo, Mzee wa Upako akajibu kwamba alikuwa anawenda kanisani kwake Ubungo Kibangu kwenye shughuli zake za kawaida za kiroho.
MADAI YA ROBERT
Madai ya upande wa Robert anayedaiwa kuongoza vijana wenzake kumfanyia vurugu Mzee wa Upako yanasema kuwa, baada ya mtiti huo wa risasi, yeye alikimbilia Kituo cha Polisi Mbezi, Dar na kufungua malalamiko yenye Kumbukumbu Na. JMD/RB/11099/2014 KUTISHIA KUUA KWA RISASI!Hata hivyo, Robert alipopigiwa simu ili kuulizwa kwa undani hakupokea  licha ya kuita kwa muda mrefu na kutumiwa meseji kwa namba yake ya simu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate