Kwako Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka.
Najua bado hujatulia kutokana na ziara ya kushtukiza ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee jimboni kwako, Muleba Kusini ambapo amemwaga ‘upupu’ kwa wapiga kura wako. Sijui lengo la ziara yake jimboni kwako ni nini lakini leo sitaki kuzungumzia hilo.
Najua bado hujatulia kutokana na ziara ya kushtukiza ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee jimboni kwako, Muleba Kusini ambapo amemwaga ‘upupu’ kwa wapiga kura wako. Sijui lengo la ziara yake jimboni kwako ni nini lakini leo sitaki kuzungumzia hilo.
Pamoja na wakati mgumu ulionao kutokana na matatizo lukuki ya ardhi
yanayokuhusu moja kwa moja kwa sababu wewe ndiye waziri mwenye dhamana
katika masuala yote ya ardhi, nataka kukufikishia ujumbe wangu kwako.
Mimi sikuzaliwa Oktoba 12, 1950 katika Kijiji cha Kangaviyo mkoani
Kagera kama wewe. Nakuapia sina CV kubwa kama wewe, sijawahi kufundisha
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1993 hadi 1998 kama wewe.
Sijawahi kupata ‘exposure’ kubwa ya kimataifa kama wewe, sijawahi
kufanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la UN-Habitat wala
sijawahi kuzunguka sehemu nyingi duniani, nikishika nyadhifa mbalimbali
kama wewe.
Mimi ni mlalahoi tu, mbumbumbu nisiyejua chochote kuhusu mambo ya
kimataifa wala serikali na utawala kama wewe. Hata hivyo, hilo
halinizuii kukufikishia ujumbe wangu kwako.
Najua kwamba wewe ni mwanamke mchapakazi, uliyesoma na mwenye uwezo
wa kuongoza ndiyo maana umeshika nyadhifa mbalimbali kwa nyakati
tofauti, kuanzia Umoja wa Mataifa mpaka kwenye Serikali ya Tanzania.
Naamini umepata uzoefu mkubwa wa namna ya kuongoza na kuzitatua kero
mbalimbali zinazowakabili watu unaowaongoza.
Hata hivyo, mbona unashindwa kuonesha uzoefu na uwezo wako katika
wizara unayoiongoza? Kuna matatizo mengi sana yanayohusu ardhi katika
nchi hii, nikianza kuyaorodhesha, gazeti zima litajaa na bado
hayataisha.
Ina maana huyajui matatizo haya? Hujui kero zinazowakumbwa wananchi
wa Mbarali kwenye shamba la mpunga la Kapunga? Huyajui matatizo ya ardhi
yanayowakabili wananchi wa Kigamboni? Vipi kuhusu mgogoro wa muda mrefu
wa Chasimba na Chatembo, Kinondoni jijini Dar es Salaam?
Vipi kuhusu mapigano ya wakulima na wafugaji katika Bonde la Mto
Rufiji na mkoani Morogoro? Ulianzisha mkakati kabambe wa kubomoa
mahekalu ya watu waliojenga kwenye fukwe za bahari na uoto wa mikoko
lakini mbona nyumba zilizobomolewa zilikuwa ni za ‘akina mwenzangu na
mimi’ tu wakati mahekalu ya vigogo bado yamesimama?
Sitaki kuamini taarifa zinazoeleza kuwa unamiliki ekari zaidi ya 800
katika Kijiji cha Kyamnyorwa wilayani Muleba katika jimbo lako. Sitaki
kuamini kama ni kweli na wewe unamiliki ekari za kutosha eneo la
Kigamboni. Naamini wewe ni mzalendo, unawapenda Watanzania na ndiyo
maana uliamua kuachia wadhifa mkubwa Umoja wa Mataifa na kurudi
kuwatumikia wananchi wa Muleba.
Lakini mbona unashindwa kuyashughulikia matatizo haya yanayowakera
wengi? Viwanja vya wazi karibu asilimia kubwa vimeshavamiwa na kujengwa
‘mijengo’ ya maana, kwa nini unalifumbia macho hili?
Kwa bahati mbaya mimi nitabaki kuwa mimi na sitaweza kuwa wewe lakini kama ningekuwa mimi kwenye nafasi yako, kwa hii migogoro ya ardhi inayoendelea nchi nzima, narudia tena kusema bila kumung’unya maneno kwamba nisingeifumbia macho, ningechukua hatua haraka sana.
Kwa bahati mbaya mimi nitabaki kuwa mimi na sitaweza kuwa wewe lakini kama ningekuwa mimi kwenye nafasi yako, kwa hii migogoro ya ardhi inayoendelea nchi nzima, narudia tena kusema bila kumung’unya maneno kwamba nisingeifumbia macho, ningechukua hatua haraka sana.
Pengine hii ndiyo ingekuwa alama kwa wananchi wangu juu ya uaminifu
wao kwangu kwa nyadhifa nyingine kubwa zaidi maana nasikia unataka
kuchukua kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Wasalaam!
Wasalaam!
CREDIT: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment