EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, December 25, 2014

ESCROW BADO MOTO

WAKATI Rais Jakaya Kikwete akiwa amemuwajibisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka kufuatia kumegewa mgawo wa fedha za Tegeta Escrow, binti anayedaiwa kuwa mwanaye, amejikuta akipata wakati mgumu baada ya kumtetea mama yake kupitia mitandao ya kijamii.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka.
Katika Mtandao wa Twitter, binti huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kagem Tibaijuka, alimtetea mama yake akisema fedha zilizowekwa kwenye akaunti yake zilikuwa ni safi na halali na kwamba ziliwekwa kwa nia njema ya kuwasaidia kielimu watoto wa kike.
“My mum did nothing wrong except wanting to help young girls get an education. A school built with my late father. Accepted a donation,” (Mama yangu hakufanya kosa lolote isipokuwa alitaka kuwasaidia wasichana kupata elimu. Shule ilijengwa na marehemu baba yangu. Mchango ukakubaliwa)yalikuwa  ni moja ya maneno yake katika mtandao huo wa Twitter.
Aidha, aliwashambulia wanawake walioonekana kushangilia wakati Rais Kikwete alipotangaza kumuwajibisha mama yake, akiwaambia kuwa anawashangaa kushangilia anguko la mwanamke mwenzao na kwamba hata wao iko siku yatawakuta ya kuwakuta.
Rais Jakaya Kikwete.
Lakini katika mitandao mingine ya kijamii, ikiwemo Facebook na Jamii Forum inayotembelewa na watanzania wengi, walimshambulia binti huyo kwa kumwelezea kama mtu aliyelewa fedha na kwamba mama yake alistahili kuondolewa kwenye nafasi yake, ikiwa ni pamoja na kushtakiwa.

Wachangiaji walioonekana kuchukizwa na utetezi wa binti huyo kwa mama yake, walisema licha ya Profesa Tibaijuka kuondolewa, pia watu wote waliotajwa, wakiwemo Waziri Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi nao walistahili kuondolewa katika nafasi zao.
Gazeti hili lilimtafuta mama Tibaijuka kupitia simu zake mbili za mkononi, ili kuzungumzia maoni yake baada ya kukutwa na ajali hiyo ya kisiasa pamoja na kumuuliza kama Kagem ni bintiye, lakini moja iliyopatikana, iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo baadaye simu hiyo ilipopigwa, ilionekana imezimwa.
Kagem Tibaijuka.
Aidha Kagem mwenyewe, ambaye ofisi zake zinadaiwa kuwa eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, naye hakupokea simu yake ya mkononi aliyopigiwa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.
Jumatatu iliyopita, Rais Kikwete alizungumzia suala hilo la fedha zilizodaiwa na Bunge kuwa ni za umma, kuchukuliwa isivyo halali katika akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania. Wakati Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema alijiuzulu mwenyewe na mama Tibaijuka kuwajibishwa, viongozi wengine waliodaiwa kuhusika na fedha hizo wanaendelea kuchunguzwa na hatua stahiki dhidi yao zitachukuliwa.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate