
Mshindi wa Big Brother ‘hotshots’ 2014, Idris Sultan kutoka Tanzania aliyekuwa akituwakilisha ndani ya mjengo huo.
Mshiriki kutoka Tanzania aliyekuwa akituwakilisha ndani ya mjengo wa
Big Brother ‘hotshots’, Idris Sultan ameibuka kidedea katika shindano
hilo usiku huu na kunyakuwa kitita cha dola 300,000 (Sawa na
510,186,000).
Tangu asubuhi Runinga ya DStv kupitia Channel 197 na 198 ilikuwa inaonyesha washiriki nane waliokuwa wamebakia katika mjengo huo, huku kamera ikimmulika zaidi Idris mara kwa mara jambo lililoashiria ushindi kwa ndugu yetu Idris.

Fainali za Big Brother ‘hotshots’ zimeanza saa 3:00 Usiku huku Idris akiwaongoza wenzake saba ambao ni Tayo (Nigeria), JJ (Zimbabwe), Nhlanha (Afrika Kusini), Sipe (Malawi), Butterfly (Zimbabwe), Ma mbea (Ghana) pamoja na Macky2 wa Zambia.
No comments:
Post a Comment