Taarifa rasmi kutoka klabu ya Yanga zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya timu hiyo baada ya uongozi wa Yanga kufikia makubaliano naye ya kuvunja mkataba.
Sababu ya maamuzi haya ni pamoja na kushindwa kukubaliana juu ya endeshwaji wa Yangu kwenye maswala ya benchi la ufundi.
Yanga ilitaka kumpa kazi ya ukurugenzi wa ufundi bwana Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo kocha Maximo hakukubaliana nalo toka mwanzo.
Sasa nafasi ya Maximo itachukuliwa na Van Der Pluijm kutoka Uholanzi. Aliwahi kuifundisha Yanga kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts ambaye pia alitoka Uholanzi.
No comments:
Post a Comment