MSANII anayefanya vizuri
katika filamu Bongo, Yusuf Mlela ambaye amekuwa akidaiwa kutumia madawa
ya kulevya maarufu kama unga, amesema utofauti wa muonekano wake kwa
sasa siyo kwa sababu ya uteja, bali inatokana na umri wake kusogea.
“Unajua mtu unavyozidi kukua na muonekano nao unabadilika, lakini
itafikia kipindi nitakuwa sawa tu hivyo naomba mashabiki wangu waelewe
kwamba mimi siyo teja na sijawahi kutumia ‘unga’ hizo ni habari za
kizushi tu,”alisema Mlela.Hivi karibuni Mlela alitupia picha kwenye mtandao wa Instagram ambapo wadau mbalimbali walionekana kushangazwa na muonekano wake na kumfananisha na mateja.
No comments:
Post a Comment