WEMA ATIMKIA GHANA
Wakati Diamond akitimkia Marekani kwenda kutumbuiza kwenye sherehe za 53 za Uhuru wa Tanganyika kwa Wabongo waishio nchini humo (Diaspora), Desemba 9, mwaka huu, Wema yeye alitimkia kwenye Mji Mkuu wa Ghana jijini Accra kuungana na Van Vicker kwa ajili ya ‘projekti’ kama ilivyokuwa kwa Diamond na Zari.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na Wema mwenyewe zilieleza kwamba yupo nchini humo kwa ajili ya kurekodi filamu huku wawili hao wakiwa ndiyo wahusika wakuu.
PICHA ZA MAHABA NIUE
Mapema Jumanne iliyopita, picha za mahaba niue za mastaa hao zilianza kuvuja kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku kila mmoja akimsifia mwenzake kuwa ni mkali.
VICKER AMSIFIA WEMA
“Nasisimka na napenda namna unavyofanya na kuipenda kazi yako. Nafurahi kufanya kazi na wewe,” aliandika Van Vicker akimsifia Wema ambaye naye alizipokea sifa hizo kwa mikono yote.
MABUSU
Baadaye waliachia picha nyingine kali zaidi ambazo ziliwaonesha wawili hao wakiwa kimahaba zaidi ambapo Wema alionekana akimbusu jamaa huyo kwa hisia kali.
KUMBE WEMA ALIPATA MWALIKO
Habari kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa Wema aliyeomba hifadhi ya jina zilieleza kwamba, hivi karibuni mwanadada huyo alipokea mwaliko wa kucheza sinema nchini Ghana kutoka kwa Van Vicker na wala hakuwa na kipingamizi kwani ni fursa aliyokuwa akiisubiri kwa muda mrefu.
“Ndiyo imetoka hivyo, sasa hivi ni mwendo wa kimataifa zaidi, hakuna kulala hadi kieleweke,” alitamba mmoja wa mameneja wa Wema na kuongeza:
“Mpango ulianza tangu kipindi kile Van Vicker alipokuja Bongo kuigiza na Mzee Chilo (Mohamed Olotu). Kilichokuwa kinasubiriwa ni mipango tu ikamilike.”
ANAMLIPIZA DIAMOND?
“Hakuna, hayo ni mambo ya kizamani, mbona ishu ilikuwepo hata kabla ya kummwaga Diamond? Unajua hizi timu ndiyo zinakuza mambo tu lakini hawayakuzi kwa ubaya, ni namna walivyo na mapenzi na msanii wao.”
TEAM WEMA VICHEKO
Katika hali ya kushtua, ghafla wafuasi wa Wema (Team Wema) waliokuwa wamezimwa na wale wa Diamond (Team Diamond) katika mitandao ya kijamii waliibuka upya.
Safari hii walikuwa wakiachia vicheko na kujisifia kwamba wao ni muziki mnene hivyo hawawezi kushindana na watoto wadogo.
“Huyo bibi bomba (Zari) si lolote. Cheki Madam (Wema) kavuka mipaka hadi Afrika Magharibi. Mtangoja sana. Sasa ni taifa kwa taifa hadi kieleweke,” ilisomeka sehemu ya maoni ya Team Wema kwenye Instagram na kupata dolegumba (likes) nyingi.
Mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi na Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady.
TEAM DIAMOND NAOKwa upande wao, Team Diamond nao walikuja juu na kuwapa makavu Team Wema kuwa watangoja sana kwani tayari jamaa siyo wa Afrika tena bali duniani kote.
VAN VICKER NI NANI?
Van Vicker amezaliwa mwaka 1977 ambapo ameoa na amejaliwa kuwa na watoto wanne.
Ni mwigizaji mkubwa barani hasa Afrika Magharibi akiwa amejijengea jina katika tasnia ya filamu nchini Ghana ya Ghollywood na Nigeria huko Nollywood akiwa ni mkurugenzi wa kampuni kubwa ya kuzalisha sinema ya Sky + Orange Productions.
AMEIGIZA SINEMA GANI?
Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Divine Love, Neat Job, Friday Night, The Hands of Time, One Night in Vegas, Total Love, When One Door Closes, Amina, Unstopable na nyingine kibao.
SINEMA ALIZOIGIZA WEMA
Akiwa anamiliki kampuni yake ya kuzalisha sinema ya Endless Fame Productions, baadhi ya filamu alizoigiza Wema ni pamoja na Point of no Return, Red Valentine, Family Tears, The Super Star, House Boy, Crazy Tenant, Basilisa, Lerato, The Diary, Tafrani, Sakata, White Maria na nyingine.
No comments:
Post a Comment