BAO pekee la Mbrazil, Andrey Coutinho limeipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Shaba katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Kombe la Mapinduzi uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Coutinho alifunga bao hilo dakika ya 86 kwa shuti kali akimaliziana krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.
Yanga SC inamaliza kwa ushindi wa asilimia 100, ikishinda mechi zake zote tatu za Kundi A, 4-0 mara mbili dhidi ya Taifa Jang’ombe na Polisi na leo 1-0.
Yanga SC inamaliza kwa ushindi wa asilimia 100, ikishinda mechi zake zote tatu za Kundi A, 4-0 mara mbili dhidi ya Taifa Jang’ombe na Polisi na leo 1-0.
Yanga SC, sasa itamenyana na JKU ya Zanzibar katika Robo Fainali kesho kutwa usiku, hapa hapa Uwanja wa Amaan.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles, Rajab Zahir, Kevin Yonean, Said Juma ‘Kizota’/Salum Telela dk59, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk81, Danny Mrwanda/Kpah Sherman dk59, Mrisho Ngassa/Amisi Tambwe dk59 na Andrey Coutinho.

Shaba FC; Bakari Shaweji, Robert Daniel, Juma Mwalimu, Bakari Kidarusi, Hassan Shaaban, Shekha Khamis, Kassim Kiondo, Suleiman Ally, Said Sinde, Mohammed Nyasa na Hamisi Ramadhani/Suma Ozil dk83.
No comments:
Post a Comment