EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, January 7, 2015

WEMA, AUNT KICHEKO KABURINI KWA NGWEA


CHANZO:GLOBALPUBLISHERS
INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au ‘waliamka’ nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!
Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.
Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.

ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililonaswa zimazima na kamera za Risasi Jumatano, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro.
ILIVYOKUWA
Aunt ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya ‘kruu’ ya Wema, akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu, Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.
CHA AJABU SASA
Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!
...Wakizidi kucheka katika kaburi hilo.
Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo, nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na ‘hamsini zao’.-
WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka. Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.
Wakati Wema akionesha ubinadamu huo, ‘mwenzangu na mimi’, Aunt yeye alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.
WEMA AJIELEZA KWA RISASI
Baada ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu, paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu ya kaburi la staa huyo.Wema: “Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”
Albert Mangweha ‘Ngwea’ enzi za uhai wake.
KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?
Awali, mastaa hao na wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa  Matei Lounge mjini Dodoma.Wakiwa wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo miongoni mwa mambo waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi la Ngwea na kuangusha dua fupi.
Hata hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo la Wema na watu wake hatimaye walifanya dua fupi ya kumuombea malazi mema Albert Mangweha.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Mangweha alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza  ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate