Stori: Gladness Mallya NENO!
 Siku chache baada ya kunasa mimba ya pili, mwigizaji Flora Mvungi 
amempa somo la uzazi staa mwenzake, Aunt Ezekiel kuwa anapaswa 
kuzingatia taratibu za kliniki, vinginevyo atapata madhara makubwa.
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Flora alisema mbali na kupunguza 
kujirusha, anamshauri Aunt aende kwa Dokta Fadhili Emily wa Kliniki ya 
The Fadhaget Sanitarium Kitengo cha Sayansi na Tiba iliyopo Mbezi Beach-
 Africana jijini Dar kwani walimsaidia sana yeye katika kumuelekeza 
namna ya kulea mimba hadi kujifungua akiwa salama.Alisema wataalam hao walimsaidia katika mimba yake ya awali na hata hii ya pili wanaendelea kumpa tiba ya sayansi asilia hivyo kama Aunt ataamua kumsikiliza na kufuata ushauri wa kutopenda starehe na kuvaa viatu virefu basi atajifungua salama.

Dokta Fadhili Emily wa Kliniki ya The Fadhaget Sanitarium Kitengo cha Sayansi na Tiba.
“Kuna dawa ambazo unapewa kuanzia hatua za awali, kamwe huwezi 
kutematema mate hovyo kama wajawazito wengine, mtoto anakua vizuri na 
hadi unafikia hatua ya kujifungua huwezi kupata kashikashi,” alisema 
Flora ambaye ni mke wa staa wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan ‘H.Baba’.Aunt ambaye kwa sasa tumbo linaonekana kuwa kubwa, amekuwa akionekana katika kumbi za starehe akijirusha akiwa na mavazi ya kihasara hali ambayo inaelezwa kuwa huenda ikamsababishia madhara kiafya.
No comments:
Post a Comment