EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, January 30, 2015

KEKI YA JOKATE KWA MILLARD AYO YAIBUA MAMBO!


‘Mtu wa Nguvu’ Millard Ayo na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifurahia jambo kwenye ‘bethidei’ yake. 
Stori: Hamida Hassan na Musa Mateja/Ijumaa
Keki iliyoandaliwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Millard Ayo ‘Mtu wa Nguvu’ imeibua mambo kwa mashabiki wao.
TUJIUNGE NA MILLARD
Ishu hiyo ilijiri Januari 26, mwaka huu ambapo Jokate alimpekea keki ofisini kwake Mikocheni jijini Dar, na kujumuika na jamaa zake kukata keki hiyo.
Kwenye pati hiyo, Millard ambaye ni mtangazaji mkali wa Vipindi vya Amplifaya na Top 20 vya Clouds FM, alidaiwa kumwalika Jokate ambaye mashabiki wao walimpa jina la Special Girl (msichana maalum).
Pia katika pati hiyo, ‘ubuyu’ ulienea kwamba Jokate ndiye aliyekaangariza madikodiko na kupakua nyumbani kwa jamaa huyo kisha akamwandalia bonge la keki.

WALISHANA KEKI, JOKATE AONA AIBU
Hata hivyo, picha zao za kimahaba wakilishana keki hiyo zilizidi kuzua gumzo huku Jokate ambaye ni mwanamitindo na mwigizaji wa sinema za Kibongo akionekana mwenye aibu.
“Wamependeza sana wakati wakilishana keki, hongera zao,” ilisomeka sehemu ya maoni lukuki kwenye mitandao ya kijamii.
JOKATE ABANWA
Ili kuondoa utata juu ya uhusiano wa Jokate na Millard, Ijumaa lilizungumza nao ambapo kila mmoja aliweka mambo hadharani.
Ijumaa: Haloo Jokate…
Jokate: Haloo Hamida (mwandishi)...mambo vipi? Ijumaa: Poa. Kuna ishu naomba nikuulize inahusiana na uhusiano wako na Millard…
‘Mtu wa Nguvu’ Millard Ayo na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifurahia jambo kwenye ‘bethidei’ yake.
Jokate: Nini tena jamani?
Ijumaa: Kuna taarifa kwamba wewe ndiye uliyemwandalia Millard pati ya birthday na bonge la keki, je, ni kweli?
Jokate: Hamna. Millard is my friend tu…
Ijumaa: Inasemekana mbali na keki uliyompelekea pia ulimpikia. Je, hii imekaaje?
Jokate: Sikumpikia yeye.
Ijumaa: Sasa ulimpikia nani?
Jokate:  Nilipika nyumbani tu, niliwapikia ndugu zangu.
Ijumaa: Vipi kuhusu keki ambayo ulimpelekea?
Jokate: Keki nilimpelekea zawadi cause anafanya vizuri.
Ijumaa: Mbona sisi tunafanya kazi nzuri na birthday zinapita hujawahi kutuletea?
Jokate: Niliamua tu.
Ijumaa: Wewe tunajua upo singo, je, yeye ana girl friend na unamjua?
Jokate: Hilo swali muulizeni yeye kwani ni kitu personal (binafsi).
Ijumaa: Hivi unajua wewe ni beautiful na yeye ni handsome?
Jokate:  Kumbe mzuri eee…hahahahaa.
Ijumaa: Basi poa mtu wa nguvu.
Jokate: Poaaa…
BOFYA HAPA KUMSIKIA MILLARD
Baada ya kumsikia Jokate, Ijumaa lilimgeukia Millard ambapo mahojiano yalikuwa hivi;
Ijumaa: Mambo Millard.
Millard: Poa mambo vipi?
Millard Ayo na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifurahia jambo kwenye ‘bethidei’ yake.
Ijumaa: Poa, kuna taarifa inasambaa kwa kasi kuwa wewe na Jokate mnatoka baada ya kukuletea bonge la keki siku ya bethidei yako. Unalizungumziaje?
Millard: Siyo kweli kama watu wanavyosema. Kama vipi wapotezee.
Ijumaa: Lakini mbona hata sisi tunasikia ni wapenzi?
Millard: Watu wanazusha tu lakini siyo hivyo.
Ijumaa: Lakini ni kweli amekufanyia pati ya bethidei na lile keki?
Millard: Kwanza haikuwa pati kihivyo. Ilikuwa ishu ndogo tu ya nyumbani. Jokate alihudhuria tu kama rafiki na siyo kama watu wanavyozusha.
Ijumaa: Mbona kuna picha za tukio zinakuonesha wewe na yeye?
Millard: Ni picha tu ila hakuna chochote.
NENO LA MHARIRI
Jokate na Millard vijana watafutaji ambapo Millard ni mtangazaji ‘jembe’ ambaye ni mfano wa kuigwa kwani amejijengea heshima kubwa ndani na nje ya Bongo hivyo kujikusanyia mashabiki wengi. Ijumaa linawapa hongera na kuwataka wazidi kupasua mawingu.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate