EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, January 24, 2015

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHAZUNGUMZIA CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA KURA YA MAONI YA KATIBA‏

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Hellen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu changamoto za utekelezaji wa sheria ya kura ya maoni ya Katiba. Kulia ni Mratibu wa Katiba wa LHRC, Anna Henga na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Ezekiel Massanja.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo


Wapiga picha na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kina wasiwasi na mchakato wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika kwa sabau ya muda mdogo ulibaki ikizingatiwa daftari la wapigakura halijafanyiwa marekebisho pia watanzania wengi hawana uelewa na katiba iliyopendekezwa.
Kituo kimetoa mapendokezo kwa Serikali kuahirisha tarehe ya kupiga kura ya maoni kwa kile kilichodaiwa katiba inayopendekezwa inamapungufu na yasiporekebishwa muda huu yanaweza kuathiri kura ya maoni na kuwakosesha watanzania wengi  kushiriki haki yao kikatiba.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, DK. Hellen Kijo- Bisimba alisema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kufuatilia mchakato wa katiba, kubaini mapugufu mengi likiwemo la muda mdogo na wananchi wengi kutoelewa vizuri katiba inayopendekezwa.
"Mchakato wa kura ya maoni unaenda kukamilika Februari 28 kwa mjibu wa sheria ya kura hiyo.Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapaswa kuboresha daftari la wapiga kura ndipo kura ipigwe, ukizingatia zimebaki siku takribani 25 kufikiaki hitimisho,sisi tunaona kuna changamoto ya muda na ni vyema zoezi hilo lisongezwe mbele,"alisema.
Aliongeza kuwa vifaa vya BRV vinavyotarajiwa kutumika kwa mara ya kwanza na tume ya uchaguzi vimeonesha changamoto katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na hivyo kituo hicho kinawasiwasi na mchakato mzima wa upatikaji wa katiba iliyo bora.
"Kifungu cha 10 katika katiba inayopendekezwa kimezungumzia vituo vya kupigia kura, kwamba vitapangwa kulingana na maeneo yaliyo na watu wengi katika maeneo husika wasiwasi wangu hapa tume inaweza kutotumia majimbo ya zamani na kutengeza majimbo mpya,"alisema.
Bisimba alisema changamoto nyingine katika mchakatio huo ni Usajili wa kamati za kura ya maoni katika kuikubali au kuikataa kura hiyo katiba inaelekeza kamati ni lazima ipeleke maombi kabla ya siku 21 kupigwa kwa kura ya maoni.
"Utaratibu ambao sisi kulingana na uzoefu wetu wa kufanya kazi tunaona haya ni masharti magumu yanayoekekezwa kwenye kamati za kura, kwani inawataka pia kueleza vyanzo vya mapato yao kitu ambacho kinaweza kusababisha  kamati zingine kutopata usajili,"alisema.
Dk.Bisimba aliongeza kuwa changamoto ambayo kituo kinaona kuwa ni kiini macho ni pale inapoelezwa kwamba wanzazibar waishio Tanzania bara wakipiga kura kura zao zitahesambiwa upande wa zanzibar.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate