EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, January 6, 2015

MWALIMU: NAONGOZA KUPIGWA NA MUME

MWALIMU Gaudencia Gitano (40) anayefundisha Shule ya Msingi Kivelu jijini Dar es Salaam, amedai huenda yeye ndiye anayeongoza kwa kupigwa kuliko wanawake wengine wote jijini, baada ya kudai anazo RB tano za vipigo tofauti kutoka kwa mumewe kwa nyakati mbalimbali tangu aolewe Oktoba 25, 2002, katika ndoa ya kiserikali iliyofungwa Ilala Boma.
Mwalimu Gaudencia Gitano (40) anayedai kupigwa mara nyingi na mume wake.
Akizungumza akiwa kitandani katika Hospitali ya Dar  Group iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Gaudensia (pichani), alidai kupigwa mara kwa mara kiasi kwamba katika vituo vya polisi na hospitali, amekuwa ni mwenyeji.
“Mimi ni mke wa pili kati ya watatu na tulifunga ndoa ya kiserikali na mume wangu Colman Marwa Oktoba 25, 2002 huko Ilala Boma. Tulikuwa tukipendana na Mungu ametujaalia tumepata watoto wawili, tulikuwa tukiishi pamoja katika nyumba yetu huko Kitunda na baadaye tukahamia katika nyumba yetu nyingine huko Msongola.
Bi. Gaudencia Gitano akiuguza majeraha ya kipigo.
“Kipigo kilianza mara baada ya kuoa mke wa tatu, kukawa hakuna amani ndani ya nyumba, kila wakati ni kupigwa, nimechoka kutoa taarifa vituo mbalimbali vya polisi na kulazwa hospitalini, nimechoka na manyanyaso, ipo siku najua ataniua, Watanzania naombeni msaada wa kisheria kabla hajaniua.

“Huu ni mtiririko wa taarifa ya mashambulio ya kudhuru mwili nilizokuwa nikifungua katika vituo mbalimbali vya polisi, kwa mara ya kwanza aliponivunja mkono mwaka 2012 nilitoa taarifa katika kituo cha polisi Staki Shari jalada Na: STK/RB/10673/2012, kipigo cha pili nilifungua jalada Na: STK/RB/12631/2012, kilifuatia kipigo kingine nikafungua jalada No. KIT/RB/1400/2012, katika kituo cha polisi Kitunda.
“Vipigo havikuishia hapo, mwaka 2013, nilipigwa karibia kufa nikatoa taarifa polisi jalada Na. KIT/RB/2976/2013 na kipigo cha mwisho cha kufungia mwaka, hadi nilipopoteza fahamu nilifungua jalada Na. STK/ RB/ 17579/ 2014.

Hali aliyokuwa nayo mwalimu Gaudencia Gitano baada ya kipigo cha mwaka 2012.
“Nakumbuka mwaka jana baada ya kuchoka na kipigo niliamua kuondoka na kupanga Kivule, alinifuata, akanipiga na kunivunja mkono, akachukua vitu vyangu vyote vya ndani, nilisononeka sana, nikanunua vingine, alirudi akanipiga na kuchukua tena vitu hivyo,” alisema mwalimu huyo kwa uchungu.
Akisimulia zaidi, alisema licha ya vipigo hivyo, ambavyo anaamini siku yoyote vitamuua, lakini mwanaume wake huyo hawajali watoto kwa chochote, si chakula, matibabu wala mahitaji ya shuleni, ambapo kila kitu anakifanya mwenyewe.
Mwalimu Gaudencia Gitano akiwa na mume wake.
“Mwaka 2012 nilifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga nikihitaji talaka, aliandikiwa barua ya wito lakini hakufika katika kesi hiyo Na: 62, kwa hivi sasa nimechoka kwani nimekuwa nikifundisha nikiwa na manundu sehemu mbalimbali za mwili, wanafunzi wakiniuliza nashindwa cha kuwajibu, nawaombeni Watanzania mnisaidie kisheria, nimeshanusa kifo.
“Nitashukuru kwa watakaojitokeza kunisaidia, nawatakieni maisha mema, nawaomba mashemeji zangu endapo Mungu atanichukua kutokana na vipigo vya mara kwa mara, muwachukue  watoto muwatunze, huyu hawezi kuwatunza.”
Mume wa mwalimu huyo, Colman Marwa alipopigiwa simu na waandishi wetu na kuulizwa kuhusu madai hayo alijibu kijeuri. “Wewe kama unataka kumuwekea wakili muweke, huwezi kuniuliza mimi au nenda kawe wakili wake,” alisema na kukata simu. 
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate