EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, January 12, 2015

SKENDO! MAMA AJIFUNGUA, MANESI WADAIWA KUMTUMBUKIZA MTOTO KWENYE NDOO

Stori: Dustan Shekidele, Morogoro No! Manesi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wameingia kwenye kashfa nzito ya kusababisha kifo baada ya kudaiwa kumtumbukiza mtoto mchanga kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.
Katoto kachanga kalikotumbukizwa kwenye ndoo kwa zaidi ya saa 3.
Tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo mkoani hapa lilijiri hivi karibuni ambapo mwanamke aitwaye Zainabu lsmali, mkazi wa Kididimo jirani na Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine ‘SUA’ alishikwa na uchungu wa kujifungua na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa msaada wa jirani yake aliyejitambulisha kwa jina la Mama Sira Manga.
Ndoo iliyotumika.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda juu ya tukio hilo, Mama Manga alikuwa na haya ya kusema: “Huu ni uzembe mkubwa wa manesi. Tulipofika hospitali mtoto alizaliwa akiwa hai lakini alikuwa njiti kwani alikaa tumboni kwa mama yake miezi 7 badala ya 9.

Ndugu wa mama akiwa na mtoto huyo.
“Cha ajabu usiku huo manesi baada ya kumcheki mtoto walisema ni wa kike lakini eti walidai amekufa hivyo waliamua kuchukua matambara ya mzazi yaliyotumika kujifungua na kumzoa mtoto huyo na kumuweka kwenye ndoo ambayo kwa kawaida sisi wazazi huwa tunakwenda nazo leba.
“Walituambia tukazike, unajua kutoka hospitali hadi Kididimo juu ya Milima ya Uluguru ni mbali na gari lilichelewa kutufuata hivyo mtoto huyo alikaa kwenye ndoo zaidi ya saa 3.

Mama wa mtoto huyo, Zainabu lsmali
“Tulipofika nyumbani na kumtoa mtoto kwenye ndoo tukamuona anahema na kufumbua macho baada ya kumtingisha akakohoa ndipo tukamkimbiza tena hospitali.
Pamoja na jitihada za manesi hao, kesho yake mtoto huyo alifariki dunia baada ya kitovu chake kuingiza hewa kwani kilikuwa bado hakijakatwa.

Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo.
Mama wa mtoto huyo, Zainabu alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema:
“Roho inauma sana lakini mzungumzaji wa tukio hilo ni mume wangu.”
Baba wa mtoto huyo, Haji Kondo alipohojiwa na mwandishi wetu alisema: “Ni kweli nimempoteza mwanangu lakini nisingependa kutoa lawama kwa manesi kwani mke wangu bado anaendelea kuzaa.”
Mwandishi wetu alifika hospitalini hapo na kuzungumza na daktari mfawidhi, Dokta Rita Lyamuya ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.

Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dokta Rita Lyamuya.
“Ni kweli tukio hilo limetokea kwenye wodi yetu ya wazazi.
“Manesi walitimiza jukumu lao la kumhudumia mzazi lakini kwa bahati mbaya tuna changamoto ya umeme kukatika bila taarifa hivyo wakati manesi wakimzalisha alijifungua mtoto njiti.
“Ghafla umeme ulikatika na kutokana na giza, manesi walijua mtoto amekufa hivyo waliwaeleza wanandugu kwamba mtoto amefariki dunia.

“Ndugu walimchukua walipofika kwao na kukitoa kwenye ndoo walibaini mtoto bado yupo hai.
“Walimleta tena hapa hospitali na tulifanya juhudi za kumtibu lakini kwa bahati mbaya amefariki dunia.”

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate