IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya mastaa wa kike Bongo Muvi wanaishi kwa kuuza miili yao, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili.
Akizungumza na waandishi wetu, msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella’, alisema wasanii wengi wanaishi maisha ya thamani wakati kiuhalisia kazi yao haiwaingizii kipato kinachofanana na maisha ya thamani wanayoishi hivyo kuamua kujiuza.
Msanii wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda ‘Bella’.
“Filamu hazilipi, wengi tunajiuza. Bajeti yenyewe ya muvi ni ndogo,
wasanii wengi wanataka kulipwa katika muvi moja, haiwezekani kumiliki
vitu vya thamani ndiyo maana tunaamua kujiuza.“Hakuna msanii anayeishi maisha ya kutegemea filamu, kwanza hazilipi kivile kama ambavyo wengi wanavyosema, ukweli ni kwamba wasanii tunajiuza ili tupate pesa ndiyo ituweke mjini tuendelee kung’aa,” alisema Bella.
Wakizungumza na waandishi wetu kwa masharti ya kutotajwa majina yao walikiri kuwa wasanii wengi wanajiuza kutokana na kutaka kuendana na hadhi ya umaarufu.
Mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’.
“Ukweli ndiyo huo, hakuna anayeweza kuishi maisha ya kumiliki magari
ya kifahari, nyumba kwa kazi ya sanaa ni uongo mtupu,” alisema mmoja wa
wasanii hao.Alipoulizwa kuhusiana na ishu ya kujiuza, mwigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ alisema: “Binafsi naishi maisha ya kawaida, najua wapo wanaojiuza, nawapa pole maana wanapenda maisha ya mteremko, mimi siyaungi mkono kabisa.”
Alipotafutwa mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’ naye alikiri: “Wasanii wengi Bongo wanategemea kuhongwa na mabwana tofauti ili wapate jeuri ya kujifanya wanazo, utakuta anatengeneza nywele za milioni mbili au kanunua nguo ya milioni kumi huo ni uongo tu, filamu hazilipi kiivyo wengi wanataka kuiga maisha ya wasanii wa nje.”
No comments:
Post a Comment