Jeneza lenye Mwili wa
marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari kushushwa nyumbani
kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho
zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili wake katika Nyumba yake
ya Milele.
Askari wa Jeshi la Polisi
Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa DCP Mstaafu wa
Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew Michael Kumalilwa wakiingia
katika nyumba yake iliyopo Tabata Segerea kwaajili ya Misa na ndugu,
jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha
katika Nyumba yake ya Milele ambapo Marehemu alizikwa katika nyumba
kwake Tabata Segerea.
Mtoto wa Kwanza wa
Marehemu Andrew Michael Kumalilwa, Patricia Andrew akiwa mwenye huzuni
wakati wa msiba wa marehemu Baba yake ambapo marehemu alikuwa mstaafu wa
jeshi la Polisi Tanzania akiwa na Cheo cha DCP.
Jeneza lililokuwa
limebeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukitolewa
katika chumba cha kuhifadhia maiti kwaajili ya kuelekea nyumbani Kwake
Segerea ambapo mazishi yalifanyika
Baadhi ya Askari wa
Jeshi la Polisi Tanzania wakitoa heshima mbele ya jeneza lililobeba
Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ambae alikuwa mstaafu wa
jeshi la Polisi kwa ngazi ya DCP
Ndugu wa marehemu
akijadiliana jambo na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Kutoa
Heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa Mzee Andrew
Kumalilwa ambae alizikwa nyumbani kwake Tabata Segerea tarehe 14
Februari 2015.
Mwakilishi kutoka Wizara
ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Simon Siro akitoa
maneno mafupi kabla ya kwenda kuupumzisha Mwili wa marehemu Mzee Andrew
Kumalilwa katika nyumba yake ya Milele. Marehemu Andrew Kumalilwa
alizikwa mnamo tarehe 14 February 2015 huko Nyumbani Kwake Tabata
Segerea.
No comments:
Post a Comment