ABIRIA zaidi ya 40 wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi la Majinja ambalo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam kufunikwa na kontena maeneo ya Mafinga mkoani Iringa muda huu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita lori ndipo walipondokewa na kontena.
Inadaiwa kuwa basi hilo lilikuwa limebeba abiria 65 na abiria nane tu ndiyo walionusurika katika ajali hiyo mbaya.
No comments:
Post a Comment