Mahakama iliyoketi chini ya Jaji Mziray, ilikubaliana na hoja za mawakili wa Chadema, waliosema kuwa ufunguaji wa kesi hiyo ulikiuka baadhi ya vifungu vya sheria na hivyo kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kulipa gharama zote za kesi hiyo.
Wakati Zitto akifungua kesi hiyo Januari mwaka juzi, tayari Chadema ilikuwa imewafukuza uanachama Dr. Kitilya Mkumbo na Samson Mwigamba ambao pamoja na Zitto, walituhumiwa kupanga njama za kufanya mapinduzi ya uongozi ndani ya chama hicho. Zitto alikuwa akitetewa na wakili Albert Msando wakati Chadema iliwakilishwa na Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Mallya.
No comments:
Post a Comment