Akizungumza na East Africa Radio Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga, Mohammed Mpinga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.
Kwa mujibu wa Kamanda gari dogo
ilikuwa likitaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na ndipo
ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga
kwenda Dar es salaam.
Baada ya basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngorika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.
Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia ni wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

(PICHA:JAMIIFORUMS)
No comments:
Post a Comment