EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, May 22, 2015

BATULI: Kanumba Kama Kaacha Laana Kwenye Filamu Za Bongo

APRILI 7 mwaka 2012 tasnia ya filamu ilipatwa na majonzi makubwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mwigizaji nguli, Steven Kanumba, ambaye alikuwa kipenzi cha wengi ndani na nje ya nchi.
Licha ya wengi kutokuamini kwa muda huo, baada ya muda ikagundulika kweli amefariki, hivyo majonzi zaidi yakarindima, huku kila mtu akisema lake kuhusu kifo hicho.


Baada ya mazishi yake mashabiki walijipa matumaini kwamba tasnia hiyo licha ya kumpoteza mwigizaji huyo ingeendelea vema kutokana na kuwa na idadi kubwa ya waigizaji wenye sifa kama za Kanumba, lakini hadi leo mwaka wa tatu tasnia hiyo inaonekana kupoteza mvuto.
Mwigizaji, Yobnesh Yussuf ‘Batuli’, alipotembelea Kampuni ya New Habari (2006) Ltd , aliongeza chachu ya kutaka kujua zaidi anamkumbukaje Kanumba ambaye waliwahi kufanya kazi kwa ukaribu.
“Wasanii wengi hatujui tatizo ni nini, ndiyo maana naweza kusema kama ameacha laana kwa kuwa tumekutana mara kwa mara kuzungumzia jambo hilo, lakini kama tumeshindwa tumejitahidi na hakuna aliyeweza kufikia mvuto na uwezo wake kwa mashabiki, ndiyo maana tunaonekana kama tunapoteza mwelekeo na kifo chake ni kama kimeacha laana kwa filamu za Tanzania,’’ anaeleza Batuli.
Batuli, mwenye watoto wawili ambaye amezaa mapema kwa hofu ya uzuri wake kuisha kabla ya kupata motto, anasema wakati mwingine wanajikuta wakisema kwamba kwa sasa wanasubiri muujiza ya Mungu ndiyo kutokee mapinduzi mapya katika filamu za bongo, maana kwa sasa hali imeyumba.

Tatizo nini?
Batuli anasema zipo changamoto nyingi zinazowafanya wasifikie mafanikio aliyokuwa nayo Kanumba katika filamu, likiwemo la kutokuaminiwa na wafadhili kunakotokana na baadhi ya waigizaji maarufu wenye majina makubwa katika tasnia hiyo kudhulumu wafadhili hao kiasi kwamba hawataki kufanya kazi na waigizaji wengine wa filamu.

“Wapo wafadhili wameshatoa fedha nyingi kwa baadhi ya masupastaa wetu ili watengeneze filamu zenye ubora na kiwango cha juu ili kuleta hamasa katika soko la filamu kama ilivyokuwa enzi za Kanumba, lakini hakuna aliyethubutu hadi leo, wengi wao wametumia kwa maslahi ya pombe, mapenzi na mambo mengine, wamesahau kwamba walipewa fedha kwa ajili ya kufanyia mapinduzi ya filamu,’’ anaeleza.
Licha ya hayo, Batuli bado anaamini kwamba Kanumba alikuwa na vitu vingi vya ziada vilivyomfanya apendwe ndani na nje ya nchi, vikiwemo uthubutu wake, kujitambua na kuwa na uchungu wa mafanikio.


“Kanumba alikuwa hakurupuki, alikuwa hakati tamaa, hata alipokuwa akichekwa aliamini ipo siku atapigiwa vigelegele, alikuwa mbunifu na mpenda kukosolewa asiye na woga wa kufanya lolote analoona ni fursa kwake,’’ anaendelea kumuelezea.
Anasema: “Kuna kipindi alikuwa anajipanga kwenda kuigiza na waigizaji wa Nigeria, aliponiambia mpango wake huo nilicheka kwamba anakwenda huko ataongea Kiingereza gani, lakini sikuamini jibu lake alisema watajua huko huko, kweli alikwenda na akaigiza na waigizaji wa Nigeria ambao ni maarufu.
“Nakumbuka tulikuwa tukikutana naye kwenye masomo ya Kiingereza, alipokwenda Big Brother watu walicheka Kiingereza chake, lakini hakukata tama, alizidi kujifunza na kujituma, hatimaye akacheza filamu ya “Moses” na mwigizaji maarufu nchini Nigeria, Ramsey Noah, tena kwa Kiingereza kizuri, kila mmoja akaikubali filamu hiyo na ujio wake wa kutangaza soko kimataifa,’’ anaeleza Batuli huku akidai kwamba ni vigumu kuziba pengo la Kanumba.

Haki miliki
Akizungumzia haki miliki, Batuli anaeleza kwamba ni jambo baya linalowaumiza wasanii kwa kuwa baadhi ya wasambazaji wananunua hakimiliki za wasanii, hivyo wakifariki dunia hukosa haki zao nyingi za msingi.
“Mfano mzuri ni kwa Kanumba, kama kungekuwa na hakimiliki ya kazi zake nadhani filamu zake zingeendelea kuuzwa na fedha zingesaidia familia yake, lakini nadhani kwa sasa hali si hivyo, ushauri wangu ni kwamba wanunuaji wa kazi za wasanii wasinunue hakimiliki za kazi zao ili wawasaidie kupiga hatua ya kimaendeleo,’’ anaeleza.

Mapenzi
Batuli anasema alikuwa anafahamu kwamba mwigizaji mwenzake, Nice Mohamed ‘Mtunisi’ alikuwa akimpenda muda mrefu lakini alikuwa mzito kumtamkia.
“Mtunisi aliniogopa, domo zege, wajanja walimuwahi lakini baada ya kusikia nimeachana na mume wangu wa mwanzo akaja kwa gia zote, nikamkubali tukawa wapenzi, lakini hatukupata mtoto,” anaeleza.
“Lakini kwa muda wote wa miaka miwili ya mapenzi yetu alikuwa akinitenda mno, alinidanganya mengi, ilifika kipindi aliniletea dada wa ndani kumbe ni mke mwezangu, nilipochunguza nikagundua kwamba ana mke aliyekuwa akiishi Kimara na pia nilisikia tetesi za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki, Pauline Zongo, nilipomuuliza alikataa.”
Anasema anakumbuka maisha ya Mtunisi kama maigizo, hakuwahi kumwambia kama alikuwa na mke, lakini alipofanya uchunguzi wake akagundua kwamba alikuwa na mke Kimara, alipomfuatilia yule mwanamke akaja moto akiwa na gazeti lake lililoandikwa habari zangu kuhusu Mtunisi, lakini baada ya kumtuliza na kuzungumza, tukatambua kwamba mwanamume huyo alikuwa akituchezea bila kujijua.
“Mtunisi alikuwa ndani, alipotoka akanipiga kibao, akidai nimekwenda kumfanyia fujo, hapo akaongeza hasira, mimi na yule mwanamke wake tulimchangia tukampiga sana, hatasahau na mapenzi yakaishia hapo, kila mtu akawa na maisha yake sina cha kukumbuka, zaidi najutia kupoteza muda wangu kwake,’’ anaeleza Batuli.

Kuasili watoto
Akielezea maisha ya kuwa na watoto zaidi, anasema anatamani watoto zaidi lakini wa kike tena wawe mapacha.
“Napenda mtoto wa kike kwa kuwa nina watoto wawili wa kiume, nitazungumza na wataalamu wa masuala ya uzazi kama nitafanikiwa sawa lakini nikishindwa nitaasili mtoto wa kike,’’ anaeleza.

Gazeti la Mtanzania,22 May 2015

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate