Mwimbaji
wa nyimbo za injili wa Columbus, Ohio Enock Mwamba(kati) akiimba moja
ya nyimbo za injili huku akiwashirikisha Mike Kalambay aliyekuja kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Upendo Nkone aliyekuja toka Tanzania
maalum kunogesha tamasha la Gospel lililofanyika siku Jumapili May 24,
2015 na kuhitimisha tamasha hilo lililokua la siku 3 mjini humo
lililoanzia siku ya Ijumaa May 22, 2015.
Mike
Kalambay akiimba huku akitoa neno la Mungu kwa Kifaransa
kilichochanganyika na lingala huku mchungaji Fayes (kulia) akitafsiri
kwa kiingereza na Kiswahili.
Mike
Kalambay akiimba moja ya nyimbo za injili kwenye tamasha la gospel
lililofanyika siku ya Jumapili May 24, 2015 mjini Columbus, Ohio.
Mike Kalambay toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akishambulia jukwaa na nyimbo za injili.
Upendo Nkone na mchungaji Donis Nkone wakifuatilia tamasha Mike Kalambay (hayupo pichani).
Mchungaji
Donis Nkone na mke wake Nnunu Nkone wakiwa wamepiga magoti wakati Mike
Kalambay akiwashukuru kwa kufanikisha ujio wake ikiwa ndio mara ya
kwanza kwa yeye kufika mjini humo.
Mike
Kalambay(kati) akipata picha ya pamoja na mchungaji Donis Nkone na mkewe
Nnunu Nkone mara tu baada ya kumalizika kwa tamasha hilo lililovuta
watu mbalimbali wa mataifa tofauti mjini Columbus, Ohio.
No comments:
Post a Comment