Magdalena Lucas enzi za uhai wake.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa majirani wa marehemu
aliyejitambulisha kwa jina la Benson Boaz alisema, imekuwa vigumu kwao
kujua chanzo hasa cha kifo cha msichana huyo aliyekuwa mfanyabiashara
ndogondogo, ingawa alikiri kuwa mara kwa mara wanandoa hao walikuwa
wakizozana kutokana na wivu uliokithiri wa mwanaume.MUME ALIKUWA NA WIVU
“Mwanaume ambaye alikuwa fundi ujenzi, alikuwa na wivu uliovuka kiwango kwa Magdalena, alikuwa akimuwekea mipaka kuzoeana hata na majirani, huyu kijana hakutaka na alipomuona mkewe anajichanganya na watu hakupendezwa kabisa,” alisema.
Jeneza lililobeba mwili wa Magdalena Lucas likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Aliongeza kuwa mara ya mwisho walimuona marehemu Ijumaa ya Mei 8
mwaka huu akiwa na mumewe lakini hawakuwaona tena na hawakuwa na shaka
kwa kuwa mlango wao ulikuwa umefungwa kwa nje.CHUMBA KUTOA HARUFU
“Jumapili jioni tukasikia chumba chao kikitoa harufu kali, ndipo tukapata hofu na kutoa taarifa polisi, walipofika na kuuvunja mlango, wakamkuta dada huyo ameuawa, akionekana kupigwa na kitu kizito kichwani maeneo ya usoni kiasi cha jicho lake kunyofoka. Hatujui kilichotokea maana hatukusikia kelele huenda kwa vile mvua nyingi ilikuwa inanyesha na mwanaume hajaonekana hadi leo,” alisema jirani huyo.
DADA HAMJUI SHEMEJIYE
Dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Asteria alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwenye familia yao kwa kuwa tangu mdogo wake aanze kuishi na Stephano, hakuwahi kuwaonesha ndugu zake.
Mwili ukiagwa kwa ajili ya mazishi.
“Tangu mdogo wangu aanze kukaa na huyo shemeji, sisi ndugu
hatukuwahi kutuoneshwa tukamjua hata kwa sura, lakini majirani walijua
kuwa ni mke wake, naumia sana, ni bora asingeamua kuishi naye kwani
hakuwa na upendo wa kweli ndiyo maana kaweza kumfanyia ukatili wa aina
hiyo,” alisema.Marehemu ambaye hakubahatika kupata mtoto, alizikwa katika Makaburi ya Tandale kwa Ali Maua lakini ndugu na jamaa hawakupata nafasi ya kuuaga mwili wake kutokana na kuharibika.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura alisema habari hizo hazijamfikia lakini atafuatilia kwa kina tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment