Beki wa timu ya taifa, Taifa Stars, Shomari Kapombe (kulia) akichuana na mchezaji wa Swaziland kwenye mchezo wao wa jana uliopigwa kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace katika michuano ya Cosafa inayoendelea huko Afrika Kusini. Stars ilifungwa bao 1-0.
Straika wa Stars, John Bocco akiruka hewani kuwania mpira na mchezaji wa Swaziland.
Kiungo
wa Stars, Erasto Nyoni akijaribu kumtoka mchezaji wa Swaziland katika
mtanange huo wa kwanza wa Stars katika michuano hiyo.
TAIFA Stars jana imeanza vibaya michuano ya Kombe la
Cosafa, baada ya kufungwa bao 1-0 na Swaziland katika mchezo wa kwanza
wa Kundi B, katika Uwanja wa Royal Bafokeng, Afrika Kusini.Matokeo hayo yanaiweka Stars inayofundishwa na Mholanzi, Mart Nooij katika mazingira magumu ya kwenda Robo Fainali baada ya Madagascar kuifunga 2-1 Lesotho katika mchezo wao wa kwanza.
Inaelezwa kuwa Nooij anaweza kuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa baada ya kufungwa mechi hiyo pamoja na matokeo mengine ya mechi zilizopita za timu hiyo.
Stars sasa lazima ishinde mechi zake mbili zijazo dhidi ya Lesotho na Madagascar ili kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali.
Bao la Swaziland lilifungwa na Sifiso Mabila kwa shuti kali dakika ya 42 baada ya kutanguliziwa pasi kwenye njia na Xolani Sibandze aliyemtoka Oscar Joshua upande wa kushoto.
Kikosi cha Tanzania; Deo Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Mrisho Ngassa/Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dk75, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Said Ndemla/Juma Luizio dk65 na Simon Msuva/Ibrahim Hajibu dk82.
Kikosi cha Swaziland; Mphikileli Dlamini, Sifiso Mabila, Siyabonga Ndluli, Sanele Mkhweli, Zweli Nxumalo/Mxlosi Lukhele dk67, Mthunzi Mkhontfo, Siboniso Malambe, Machawe Dlamini, Njabulo Ndhlovu/Sifiso Nkambule dk62, Tony Tsabedze na Xolani Sibandze/Sabelo Ndzinisa dk80.
No comments:
Post a Comment