EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, October 21, 2015

Mwalimu mkuu, mzazi wanaswa

FUMANIZI (3)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar na mwanamke huyo.
Mwandishi Wetu 
DUNIANI kuna mambo! Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita alinaswa live ofisini kwake akiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mzazi wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, kisa kikitajwa ni maandalizi ya kuivunja amri ya sita ya Mungu, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Tukio hilo la kufedhehesha, lilishuhudiwa na makamanda wa Global Publishers Kitengo Maalum cha Operasheni Fichua Maovu (OFM) ambapo pia watu wengine kadhaa walijionea kioja hicho cha mwaka.
FUMANIZI (2)HIVI NDIVYO ILIVYOANZA
Awali, Kamanda wa OFM akiwa kazini, alipokea simu kutoka kwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, akimfahamisha juu ya hali isiyo ya kawaida kwenye ofisi za mwalimu huyo zilizopo ndani ya geti la shule, kwani aliwaona askari polisi wakihaha kama wanaotaka kuzuia uhalifu.
“Jamani OFM, njooni hapa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa. Kama kuna ishu, naona askari wapo na pia ndani kwa mwalimu mkuu kama kuna ishu. Sijui ni nini!” kilisema chanzo hicho.Mara moja, kamanda huyo alifanya mawasiliano na wenzake waliokuwa ‘fildi’ na kuwafahamisha kuhusu ishu hiyo. Wakitumia pikipiki zao ‘zinazopaa’, makamanda hao walifika eneo la tukio dakika chache baadaye na kukuta mambo ndiyo kwanza yanaanza.

FUMANIZI (1)ENEO LA TUKIO
OFM walijitambulisha kwa askari waliokuwa eneo hilo na kuomba kwanza kupata picha kadhaa za kumbukumbu kabla ya maelezo, ndipo ndani ofisini, walimuona mwalimu huyo akiwa na taharuki huku akionekana kurekebisha vizuri suruali yake. Mbele yake alikuwepo mwanamke aliyejiziba uso kwa kutumia kiganja cha mkono mmoja.
SIKILIZA UTETEZI
Alipotakiwa kutoa maelezo ya kitu kilichokuwa kinaendelea ndani ya ofisi yake, mwalimu huyo alisema mwanamke aliye mbele yake alikuwa akitaka kumbaka, kwani aliingia ofisini humo na kuanza kujichekeshachekesha hovyo.
“Mkamateni mzazi huyo, anataka kunibaka. Kaja hapa, akaanza kujisemeshasemesha na kunifungua suruali yangu. Wakati namshangaa ndiyo nyinyi mnaingia,” alisema mkuu huyo huku akiichukua simu yake na kuonekana kama anayefuta kitu.
MWALIMU AWAKALISHA CHINI OFM, ASKARI
Hata hivyo, muda mchache baadaye, mwalimu huyo aliwaomba askari na makamanda wa OFM kukaa chini na kuyamaliza mambo hayo ili yasifike mbali.
“Jamani nyinyi ni wanaume wenzangu, mimi naomba tukae chini tuyamalize haya mambo hapahapa.”
OFM na askari hao walikataa mazungumzo hayo kwa vile kitendo cha mzazi huyo kukutwa ofisini muda huo ni chenye maswali mengi huku majibu yakiwa kiduchu.
MZAZI WA MWANAFUNZI ANENA
Akizungumza eneo la tukio, mzazi huyo (jina kibindoni), alisema kwamba alikuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa mwalimu huyo, akimtaka kimapenzi, jambo ambalo mara zote alikuwa akilikataa.“Huwa ananitaka, amekuwa akisema eti nikimfanikishia suala lake atahakikisha mwanangu anasoma vizuri. Sasa mimi hadi nimechoka. Wakati mwingine nilimdanganya nimesafiri. Siku moja nilifika hapa almanusura afanikishe kama siyo mlango wa ofisi kugongwa.”
USHUHUDA MZITO
Mwanamke huyo alisema siku hiyo alifika ofisini hapo baada ya kumuita, akimweleza kuwa alihitaji kuzungumza naye juu ya maendeleo ya mtoto wake. Hapo alipinga madai ya mwalimu huyo kuwa, alitaka kumbaka.
“Aaa! Kwa hili hawezi kukataa. Hata tukienda kwenye kampuni ya simu ninayotumia, tukaomba watutolee karatasi za kumbukumbu za nyuma (printout) simu ambazo tulikuwa tunapigiana utaona kwamba, alikuwa na mawasiliano na mimi ya muda mrefu sana. Kwa hilo asikatae, mimi sikutaka kumbaka ila yeye ndiyo alilazimisha penzi hapa ofisini.”
Wakati mwanamke huyo akitoa ushuhuda huo, mwalimu huyo alikuwa akisikiliza kwa umakini huku akiendelea kusisitiza utetezi wake.
MWALIMU APIGWA PINGU, OFM YAONDOKA
Baada ya hapo, OFM iliondoka ofisini hapo wakati mwalimu huyo akipigwa pingu. Na kwa mujibu wa askari, walikuwa wakienda kwenye kituo cha polisi kilicho karibu na eneo la tukio.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate